
Bendi ya muziki wa Taarabu ya Zanzibar jana usiku wa kuamkialeo ilikonga nyoyo za wapenzi wa muziki huo pale walipofanya onyesho lao katika ukumbi Traveltine. Bendi hiyo iliyojizolea umarufu Afrika Mashariki na kati na huko katika bara la Ulaya, kundi hilo la muziki wa Taalabu lilianzishwa mwaka 1905 huko Zanzibar. Kiongozi wa kundi hilo Nasoro Issa Matona ambaye ni mtoto wa marehemu Issa Matona aliyefariki Dunia mwaka 2005 kwa kugongwa na gari wakati akie leke kwenye onyesho katika ukumbi wa Diamond Jubilee alisema kuwa kundi lao linapendwa sana kwa sababu ya kuimba nyimbo asilia zinazotokana na uafrika halisi. Kwa sasa kundi hilo lipo jijini Dar es Salaam ambapo wanategemea kufanya maonyesho kadhaa.

1 comment:
Thnx 4 da pics, I was looking 4 them, I wish I was there.
Post a Comment