Welcome to pwaniraha blog please contribute by posting your comments on our blog, kindly note that abussive language is strictly not entertained. Thank you.
Welcome To Pwani Raha Blog; email us at "pwaniraha@gmail.com"

April 3, 2009

WALIOWEKEZA HELA ZAO DECI KUNA HATARI WAKAZIKOSA

DECI (T) Limited ni kampuni ambayo Watanzania wengi walikuwa wanawekeza hela zao kwa ajili ya kupata riba. Cha ajabu ni kiasi cha riba kinachotolewa na DECI. Kwa mahesabu ya haraka riba ikanuwa takriban asilimia 100% ndani ya wiki 17 tu ya kiasi ulichowekeza, kwa maneno mengine ni kuwa unaweza kuwekeza Tsh. 200,000 ukapata 500,000 ila kuna makato ambayo hayazidi laki moja. Wazungu wanasema "When the deal is too good to be true, think twice".

Hapa maswali ya kujiuliza ni yafuatayo;
1. Hivi inakuwaje DECI wanatoa riba ya zaidi ya 100% ndani ya wiki 17, wao hizo riba wanazizalishaje au wanaziwekeza wapi, ni biashara gani inaweza kukupa faida hiyo. Hebu nichambue kidogo. Riba kubwa ninayoifahamu ni ile inayotolewa na Benki Kuu kwa mfumo wa "Treasury Bill" au "Bonds" ambapo tangu mwaka huu uanze riba ya juu imewahi kufika 14%-15% kwa mwaka. Iweje DECI walipe 100% kwa wiki 17 ( 100 x 3= 300% riba kwa mwaka), wao wanazizalisha wapi?.

2. Kampuni nzima ya uwekezaji wana email ya YAHOO (decitanzania@yahoo.com). hawana mtandao.
3. Number za simu za kampuni hiyo ni za simu za mkononi.
4. Hii inaitwa pyramid scheme ama ponzi scheme. Pesa za wanachama wapya hutumiwa kuwalipa wanachama wa zamani, mzunguko huu hutegema sana wanachama wapya. Biashara aina hii hufikia ukingoni na wanachama kushindwa kulipa maana hakuna kinachozalishwa bali mzunguko wa fedha za wanachama.
5. Kufanya Pyramid schemes au ponzi schemes ni hatia kisheria katika marekebisho ya penal code 2006. Hata huko nchi za zilizo endelea biashara hii huwa ni marufuku, Charles Ponzi alifungwa huko Marekani kwa kosa kama hili miaka ya 1920s ambapo jina hili la Ponzy Scheme lilipoanzia.

TAHADHARI
Benki Kuu pamoja na Mamlaka ya Masoko ya awali ya hisa wametahadhari wananchi wasijingize kwenye mtego. Uchunguzi wa kina umeanzishwa dhidi ya DECI.


Chini ni maelezo yaliyomo kwenye vipeperushi vya DECI kama inavyoonekana kwenye picha ya juu kabisa ila haionekani vizuri.

.....................................................TANZANIA OFFICE
.....................................................MABIBO MWISHO
.....................................................MAMA KIWIA'S HOUSE
.....................................................PLOT NO.981
.....................................................P.O. BOX 6493
.....................................................DAR ES SALAAM
.....................................................Mobile 0713-418297/0787-010879
.....................................................0762-539064
.....................................................Email: decitanzania@yahoo.com

.......................VUNA TOKANA NA MBEGU ULIYOPANDA

KIWANGO CHA CHINI
Thamani ya Mbegu ...Fedha itakayopandwa ..Muda wa Kuiva ..Muda wa Malipo
Itakayopandwa ..................................................................................Kuanzia
10,000 .........................25,000 ...........................Wiki ya 8 ................Wiki ya 9

KIWANGO CHA KATI
Thamani ya Mbegu .Fedha itakayopandwa ..Muda wa Kuiva .....Muda wa Malipo
.....Itakayopandwa .................................................................................Kuanzia
......20,000 ............... ..50,000 ............. .........Wiki ya 12 ..............Wiki ya 13
......40,000 ..................100,000 ......................Wiki ya 12 ..............Wiki ya 13
.....60,000 ...................150,000 ......................Wiki ya 12 ..............Wiki ya 13
......80,000 ...................200,000 ......................Wiki ya 12 ..............Wiki ya 13
....100,000 ................. .250,000 ......................Wiki ya 12 ..............Wiki ya 13

KIWANGO CHA JUU
Thamani ya Mbegu ..Fedha itakayopandwa ...Muda wa Kuiva ....Muda wa Malipo
....Itakayopandwa ..............................................................................Kuanzia
....120000 .....................300,000 ........................Wiki ya 16 ..........Wiki ya 17
....140000 .......................350,000 ........................Wiki ya 16 .........Wiki ya 17
....160000 .......... ............400,000 .......................Wiki ya 16 ......... Wiki ya 17
....180000 ........... ...........450,000 ........................Wiki ya 16 .........Wiki ya 17
....200000 ............ ..........500,000 ........... .............Wiki ya 16 .......Wiki ya 17

MAELEKEZO MUHIMU KUHUSU TUSHIKAMANE REVOLVING FUND (T.R.F)
1. Kiingilio katika T.R.F.i.e. Tushikamane Revolving Fund ni Shs 20,000/=na hizi hazirudishwi.
2. Mshiriki atapanda, atavuna na atarudisha mbegu shambani siku atakapovuna.
3. Mshiriki atakachovuna baada ya kurudisha mbegu shambani kitakuwa ni halali yake wala haina riba au marejesho yoyote.
4. Maafa au chochote kitakachositisha ushiriki wake atakayestahili haki juu ya mshiriki huyo ni mrithi aliyeandikishwa wakati wa usajili.
5. Mapato/mavuno yako yanawezakupitia benki. Kitika Akaunti ya muhusika.
6. Hata iweje, fedha haitalipwa bilakitambilisho na stakabadhi (risiti) inayoonyesha siku/tarehe ya kulipwa
kama ilivyoonyeshwa katika jedwali la makumbusho.
7. DECI itatoa ushauri wa kibiashara, mafunzo ya ujuzi wa biashara, namna ya kuanzisha biashara na miradi ya maendeleo katika jamii.
8. Kiwango cha juu cha kupanda mbegu ni T.sh 200,000/= na si zaidi ya hapo.
9. Kampuni ina mamlaka ya mwisho kubadili sheria kwa wakati wowote inpoona inafaa kwa faida ya washiriki na kampuni.
10. Kila atakapovuna kiasi chochote, atakachochukua atakatwa 15% ikiwa ni gharama ya uwezeshaji wa Tushikamane Revolving Fund pamoja na kodi mbalimbali za serikali.

TUNAMTUMIKIA MUNGU KAMA FEDHA IPASAVYO KUTUTUMIKIA

No comments: