 Marehemu Rashid Lema akichechemea huku akisaidiwa na mtuhumiwa mwenzake (ambaye yuko huru sasa) alipokuwa anatoka mahakamani Februari 3 mwaka huu.
Marehemu Rashid Lema akichechemea huku akisaidiwa na mtuhumiwa mwenzake (ambaye yuko huru sasa) alipokuwa anatoka mahakamani Februari 3 mwaka huu..
SHAHIDI muhimu katika kesi ya mauji ya wafanyabiashara watatu kutoka Mahenge mkoani Morogoro na dereva taxi mmoja DC Rashid Lema amefariki dunia leo alfajiri katika hospitali ya saratani Ocean Road jijini Dar es Salaam. Taarifa zilizopatika katika hospitali hiyo kupitia Mkurugenzi wa Tiba hospitalini hapo Dk. Hamza Maunda alisema Lema alifariki majira ya saa kumi alfajiri ambapo alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa saratani. Habari zilizofikia mwandishi wa habari hii inasemekana kuwa taratibu za mazishi zinafanyika nyumbani kwake Osterbay jijini Dar es Salaam. 
.
.
DC Lema ambaye alikuwa shahidi namba 11 katika kesi hiyo inayohusisha watu 13 ilisemekana kuwa alikuwa ni shahidi muhimu kutokana na maelezo ambayo yangetoa mwanga wa kuchukuliwa kwa hatua ya kesi hiyo. Kutokana na taarifa ya Kamati ya Rais Jakaya Kikwete ambayo iliongozwa na Jaji Mstaafu Musa Kipenka Lema alitoa ushirikiano ambao ungesaidia
kurahisha maamuzi ya kesi hiyo. Inasekana kuwa DC Lema alifanikiwa kupata nguvu
katika siku za hivi karibuni ikiwa ni baada ya kuhamishwa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili na kuhamishiwa Ocean Road ambayo inajihusisha na magonjwa ya saratani. Aidha inasemekana kuwa kutokana na kifo hicho upande wa mashitaka unaweza kutumia taarifa iliyotolewa na Lema kwenye kamati ya Jaji Kipenka.

Kutokana na ugonjwa ambao ulikuwa ukimsumbua mshitakiwa huyo wa 11 mahakama iliamua kuarisha kesi hiyo kwani maelezo yake yalikuwa yakihitajika zaidi kabla ya kuanza kwa utetezi
kutoka kwa washitakiwa ambao wapo hadi leo gerezani. Kesi hiyo inawahusisha washitakiwa ambao hadi sasa wamefikishwa mahakamani ni Abdallah Zombe, SP Christopher Bageni, ASP Ahmed Makelle, WP4593 PC Jane Andrew, CPL Emmanuel Mabula, D8289 PC Michael Sonza, D2300CPL Ebeneth Saro, D.9312D/C Rashid Lema, D4656C/CPL Rajab Bakari na D.1367D/CPL Festus Gwabisabi. Washitakiwa hao ni zombe,Bagenda,Makele,WP 4513 Jane D 1406 Mabula,D8289 Michael,D2300Abeneth,B1321 Rashid Leme Mpaka sasa taratibu za mazishi zinafanyika nyumbani kwao oysterbay ambako ndipo alipokuwa akiishi.
.
Kutokana na kushindwa kwake kufika mahakamani kulisababisha shahidi wa 12 katika kesi hiyo
inayomuhusu aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam Abdallah Zombe na wenzake tisa na DC Rajab Bakari kutotoa ushahidi wake na kesi hiyo kusimamishwa hadi Lema atapotoa utetezi wake. Wakili upande wa utetezi Denis Msafiri alisema DC Bakari haruhusiwi kutoa maelezo kabla ya DC Lema kwa kuwa kuna maneno ambayo ni lazima mshitakiwa wa 11 ayatamke kwanza kwa kinywa chake ndipo shahidi mwingine aendelee. Msafiri aliyasema hayo mbele ya Jaji wa Mahakama ya Rufaa Salum Masatti baada ya kuieleza mahakama kuwa afya la DC Lema haimruhusu kufika mahakamani kutoa ushahidi na akaimbo mahakama ili ahirishe shauri hilo hadi atakapopata nafuu. "Mheshimiwa Jaji kama nilivyoomba jana mahakama yako inipe nafasi ya kwenda kuonana na mshitakiwa wa 11 kama anaweza kufika hapa kutoa ushahidi nilifanya hivyo lakini hali yake bado hairidhishi hivyo hawezi kuja kutoa ushahidi mahakamani hapa leo wala kesho.Hivyo naomba shauri hili liahirishwe," alisema Wakili Msafiri baada ya Jaji Masati kumpa nafasi.

No comments:
Post a Comment