Welcome to pwaniraha blog please contribute by posting your comments on our blog, kindly note that abussive language is strictly not entertained. Thank you.
Welcome To Pwani Raha Blog; email us at "pwaniraha@gmail.com"

April 3, 2009

SPECIAL OLYMPICS TANZANIA

1. MAFUNZO KWA MAKOCHA – TAREHE 6 – 9 APRILI 2009.

Mafunzo haya ni kwa makocha wapya 21 kutoka mikoa ya temeke, kinondoni na ilala. kila mkoa utaleta makocha 7. lengo la mafunzo haya ni kuongeza idadi ya makocha watakaoweza kufundisha michezo kwa watu wenye ulemavu wa akili kwa kuwa baadhi ya sheria za michezo hiyo zimerekebishwa ili kuwawezesha watu wenye ulemavu wa akili kucheza michezo husika. Mafunzo yatafanyika katika uwanja wa uhuru wa nje na wa ndani. michezo itakayohusika ni mpira wa miguu, riadha, mpira wa mikono na mpira wa wavu. mafunzo yataanza kila siku saa 2.00 asubuhi hadi saa 11.30 jioni. Wakufunzi wa mafunzo haya wanatoka katika jeshi la polisi ambalo limejitolea kuisaidia special olympics baada ya kuona umuhimu wa kusaidiana na jamii katika maendeleo yao. Jeshi la polisi linatambua kuwa watu wenye ulemavu wa akili ni sehemu muhimu ya jamii ambayo inastahili kushirikishwa katika huduma zote, ikiwemo michezo. wakufunzi hao ni wataalamu wa michezo watakayofundisha. hawa ni:

- Asp Jonas na insp. Mfaume watakaofundisha mpira wa miguu
- Insp Pascal atafundisha mpira wa kikapu na wa wavu
- Insp Mshinde atafundisha mpira wa mikono
- Coplo palangyo atafundisha riadha

2. Michezo Modogo (Mini Competition)
Tarehe 9 aprili 2009 kutakuwepo mashindano ya timu kutoka mikoa ya ilala, temeke na kinondoni, yatakayofanyika katika uwanja wa uhuru. michezo itakayoshindaniwa ni mpira wa miguu na riadha. mashindano yataanza saa 2.00 asubuhi hadi saa 7.00 mchana ili kupisha machezo wa mpira wa miguu, ligi ya vodacom ambao umepangwa kufanyika katika uwanja huo.

3. Mashindano Ya Taifa
Mashindano hayo yamepangwa kuanyika mkoani dar es salaam mwezi desemba 2009 (tarehe zitatajwa baadaye). mashindano haya makubwa yatashirikisha jumla ya wachezaji 500, makocha 100, wanafamilia 200 na valantia 100. wachezaji watatoka katika mikoa yote ya nchi tanzania bara na zanzibar italeta timu moja. jumla ni mikoa 24.
michezo itakayoshindaniwa ni mpira wa miguu, mpira wa wavu, riadha, mpira wa kikapu na netiboli. mashindano haya yatakuwa ni ya siku 5.

4. Mkutano Wa Waratibu Wa Mikoa
umeandaliwa mkutano wa kazi kwa waratibu wa mikoa yote 24 utakaofanyika dar es salaam tarehe 28 na 29 aprili, katika uwanja wa uhuru. katika mkutano huu, pamoja nakujadili masuala ya uendeshaji wa shughuli za special olympics, waratibu hawa watafundisha namna ya kutumia vifaa na fomu mbalimbali kwa ajili ya kurahisisha na kuweka sahihi kazi za special olympics ili tanzania iweze kwenda sawa na nchi nyingine duniani. Special olympica tanzania inawaalika waandishi wa habari na vyombo vyote vya habari katika matukio haya. aidha inashukuru kwa ushirikiano inaopata kutoka vyombo vyote vya habari.


FRANK L. MACHA
MKURUGENZI WA TAIFA
SPECIAL OLYMPICS TANZANIA

No comments: