
 Machinga Complex jinsi inavyoonekana kwa karibu, sehemu hii ina eneo kubwa la kuegesha magari na kwa ujumla ni safi na ya kuvutia. Tuombe Mungu sehemu hii itunzwe vizuri isijegeuzwa kuwa kama sehemu ya kuuza mkaa (makaa).

 Jengo hili la Machinga litakuwa na jumla ya vibanda 1,500 ambavyo kila kibanda kimoja kitagawiwa wamachinga 6. Pichani ni kibanda mojawapo ambacho kitamiliwa na wamachinga sita. Walio ndani ya kibanda hichi sio wamachinga bali wanaonyesha mfano wa jinsi mambo yatakavyokuwa biashara kitakapoanza.

Hapa wanaonyesha jinsi wamachinga watakavyokuwa wakichapa kazi zao.

Baadhi ya watu wameonyeshwa na kutoridhishwa kwao na nafasi zilizo pangiwa. Wanasema kuwa nafasi hizo ni ndogo kwahiyo wamachinga watapata shida, hata kugeuka itakuwa tabu.

Mussa Azan Zungu akiongoza kikao leo hii mjengoni hapo kujadili jinsi wamachinga watakavyo gawawi nafasi. Mengine yaliojadiliwa ni pamoja na miundombinu ya maji taka na maji safi na uwepo wa umeme wa TANESCO. Hadi sasa jengo hilo halijawekwa umeme kutokana na deni la awali la Tsh milioni 50 zinazodaiwa kwa mmiliki wa awali.

Kulia ni mchoraji ramani wa jengo hilo Bw Ernest Mhina katikati ni Bw Madanga Said mjumbe wa bodi ya ujenzi na katibu wa VIBINDO, kushoto kabisa ni mbunge wa Ilala Mhe Musa Azan Zungu.
 
No comments:
Post a Comment