Welcome to pwaniraha blog please contribute by posting your comments on our blog, kindly note that abussive language is strictly not entertained. Thank you.
Welcome To Pwani Raha Blog; email us at "pwaniraha@gmail.com"

June 1, 2010

Chuo cha Urembo kiitwacho ‘PURE’chazinduliwa Dar.

Meneja Uhusiano wa kampuni ya JWT Tanzania Barnabas Rugisha akimwelekeza kitu Mwandaaji wa mkutano wa Utambulisho wa Chuo Kipya hapa nchini kinacho husika na mafunzo ya urembo kiitwacho PURE Pure Academy of Aesthetics Limited Prashant Powar (kulia) hafla hiyo imefanyika katika hoteli ya Double Tree iliyopo jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Wandishi wa Habari wakiwa katik utambulisho huo wa Chuo hicho kinacho husiana na mafunzo ya Urembo.

Mshauri wa Chuo cha Pure Academy of Aesthetics Limited,Hanif Virani kutoka nchini Canada (kushoto) akieleza shughuli zinazotolewa na chuo hicho wakati alipokuwa akitambulisha chuo hwa Wandishi wa habari,waliokaa wa kwanza kutoka kushoto ni Muasisi wa chuo hicho Yasmini Shariff wa pili ni Mratibuwa masuala ya jinsia katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Winifrida Rutaindurwa, watatu ni Laila o Laila kutoka Kenya na Whitney MacCathy kutoka Canada. Chuo jicho kinategemea kuanza kutoa mafunzo ya urembo mwezi wa Nane mwaka huu.Afisa Habari wa kampuni ya JWT Glory akiingia katika Hotel ya Double Tree iliyopo Msasani wakati wa hafla ya mkutano wa utambulisho wa Chuo cha Pure Academy of Aesthetics Limited ambacho kinajihusisha na masuala ya mafunzo ya urembo.

Wageni waalikwa waliohudhuria mkutano wa utambulisho wa chuo cha Pure Academy of Aesthetics Limited kinachojihusisha na mafunzo ya urembo kikiwa chuo cha kwanza hapa nchini wakipata msosi katika Hoteli ya Double Tree iliyopo maeneo ya Msasani karibu na Slip Way jijini Dar es Salaam.

No comments: