Ni wazi sasa kwamba ushindani mkubwa uliopo nchini katika sekta ya simu za mkononi umeongeza nafuu kwa watumiaji kutokana na maboresho yanayofanywa na kampuni za simu za mkononi kila kukicha. Awali kampuni hizo wakati zinaingia nchini,zilikuwa zikitoza bei kubwa kwa kila muda wa maongezi,kiasi cha kumtoza hata mpokeaji badala ya mpigaji. Lakini sasa,hali imebadilika.Kila kampuni ya simu za mkononi inajitahidi kuboresha huduma zake kwa wateja kiasi kwamba mteja anaweza akaongea na ndugu na jamaa zake kutwa nzima kwa gharama ya shilingi 1 kwa sekunde tu. Gharama hiyo kwa kiasi kikubwa itawasaidia sana wafanyabiashara wakubwa na wa kati,wenye mtandao mkubwa washika dau na wateja wa bidhaa zao.
Lakini pia, hatua hiyo, itaweza kusaidia sana katika sekta ya habari na mawasiliano na hasa katika vyumba vya habari,ambako ripota sasa ataweza kuongea na kutuma taarifa kwa mhariri wake,yeye akiwa nje ya chumba cha habari. Ni katika ushindani huo, kampuni ya Vodacom Tanzania, imeanzisha huduma mpya ya kupiga simu itakayowawezesha wateja wa simu wa kampuni hiyo kupiga simu kwa kiwango cha shilingi moja kwa sekunde kote nchini. Hii inamaanisha kwamba zaidi ya wateja milioni saba wa kampuni ya simu ya Vodacom nchini watanufaika na huduma hii mpya ya malipo itakayokuwa endelevu na sio kwa kipindi maalum ‘Promosheni’. Kiwango hiki cha malipo kwa watumiaji wa simu wa Vodacom Tanzania ni muendelezo wa utolewaji wa huduma na promosheni zinazoambatana na zawadi mbalimbali ambazo huwafanya watumiaji wake kuwasiliana kwa urahisi.
.
Akizindua huduma hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Vodacom Foundation Mwamvita Makamba, alisema kuanzishwa kwake kutaongeza mabadiliko kwenye sekta ya mawasiliano nchini Tanzania.
“Kwa mtazamo wa wengi ni jambo lisilowezekana kwamba Vodacom inayoonekana kutoza huduma zake kwa viwango vya juu sokoni kuamua kutoa huduma zake kwa gharama za chini na kuweza kuziendeleza zingine kwa lengo la kurahisisha mawasiliano,” alisema Makamba. “Vodacom Tanzania inachukua fursa hii kuwashukuru wateja wake wote kwa kuendelea kuwa wateja wa Vodacom kwa kipindi chote hiki cha miaka tisa ya huduma hapa nchini na inawashauri waendelee kutumia huduma na bidhaa zetu mbalimbali na hasa huduma tuliyoizindua leo ya ”alisema. Makamba alifafanua kwamba huduma hii ni muafaka kabisa kwa wanavikundi mbalimbali vya uzalishaji mali, wafanyabiashara wadogo wadogo na wa kati,wakulima, wanafunzi,wafanyakazi pamoja na familia zetu.
Licha ya kuitambulisha huduma hiyo, Vodacom Tanzania inaendelea kutoa promosheni zake zingine kama Cheka Time na Vodajamaa. Kwa watumiaji wa Vodacom wanaojiunga na huduma ya Cheka Time wanajipatia dakika za bure za maongezi kwa gharama zinazoanzia shilingi 200/- hadi 2,000/-. Mteja anayejiunga kwenye promosheni ya Cheka kwa 200/- anapata muda wa maongezi wa dakika 15. Huduma hii ni maalum kwa watumiaji wwa mkoa wa Pwani pekee. Hata hivyo katika mikoa mingine ambapo huduma hii inapatikana imewafanya wateja kuwa katika muonekano mwingine. Vodacom atazimaliza dakika 100 au 300 za bure kabla ya muda wa siku mbili basi anaweza kujisajili na kupata dakika nyingine za BURE.
.
Aidha kwa gharama ya Cheka ya shilingi 500/- wateja wa Vodacom wanapatiwa dakika 60 za maongezi wanazoweza kuzitumia siku nzima ambapo kwa wanaopjiunga kwa shilingi 2,000/- wanapata dakika 100 wanazoweza kuzitumia kwa siku mbili. “kwa kweli sisi ndiyo tutakaofaidika zaidi. Watu walikuwa wanashindwa kuongea na ndugu zao walioko mkoani,kwa sababu kabla ya huduma hii,ya kuongea kwa shilingi moja kwa sekunde nilikuwa naweza kuongea na watu wawili au watatu tu,tena kwa ufupi…sasa kama naweza kuongea kwa shilingi moja kwa sekunde je unataka Mungu akupe nini,”anasema Angaza Geoffrey.Leornad Ephraim,ambaye pia ni mteja wa Vodacom na mkazi wa Mlalakuwa,Dares Salaam,yeye hakusita kuipongeza Vodacom kwa kuwajali wateja wake,na hasa katika kipindi hiki wanachokabiliwa na kipindi kigumu cha maisha. “Ingawa sina marafiki wengi sana wa kuwapigia,lakini nawapongeza Vodacom kwa kweli.Ninaweza kuongea hata na mama yangu aliyeko kijijini kutwa nzima,atajisikia vizuri kwa sababu atajiona kama niko naye karibu,”anasema Leornad.
Mkurugenzi mkuu wa biashara wa Vodacom Tanzania na Mkurugenzi Mkuu wa Uhusiano Mwamvita Makamba wakiongea jambao katika moja ya mikutano na wandishi wa habari
1 comment:
bape outlet
golden goose sneakers
off white
supreme hoodie
bape clothing
golden goose sneakers
yeezy 500
jordan retro
paul george shoes
supreme clothing
Post a Comment