Makamu wa Rais Dr. Ali Mohamed Shein akizindua kitabu kilichotungwa na wanasheria wanawake wakati wa Maadhimisho ya sherehe za kuazimisha miaka 20 ya Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, ambapo maandamono yalianzia katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Kushoto kwake ni Mweneyekiti wa chama hicho TAWLA Maria Kashonda akishuhudia uzinduzi huo.
Wasanii wakundi la Survivol Sisters( kutoka kulia)Latifa Abdarah,Irene Malekele na Luce Samson wakiwa miongoni mwa wanawake walioalikwa katika maadhimisho ya sherehe hizo. Wasanii hao leo wameuambia mtandao huu kuwa kuanzia hivi sasa wamesimamisha shughuli za muziki ikiwa ni sehemu ya kupumzisha akili kwanza hadi hapo baadaye kidogo.
Mmoja wa aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha wanawake wanasheria Tanzania TAWLA Hamida Shekha akiwa ameshikilia cheti chake baada ya kukabidhiwa na Makamu wa Rais DKT. Ali Mohamed Shein kwa kuwa kiongozi bora. kushoto ni mwanachama mwenzake ambaye naye alikuwa mwanasheria lakini kwa sasa amestafu Elizabeth Magamba.
Meneja wa kinywaji cha Grand Malt Consolata Adam akielezea namna wanavyotoa huduma ya kinywaji hicho kwa wateja wake wakati walipokwenda kukitangaza katika ufukwe wa coco beach hapo jana. Kinywaji hicho hakina kilevi na kinanywewa na rika zote za watanzania chupa moja huuzwa shilingi 1,000 tu.
No comments:
Post a Comment