Mkurugenzi Bw Emmanuel mwakabana akielezea jambo baada ya uzinduzirasmi wa kijiji hicho.
Mandhari ya ndani ya kijiji cha pool.
Sehemu ya mbele ya kijiji hicho.
.
Mchezo wa pool kujizolea mashabiki lukuki kutokana na kuchezwa na wengi katika maeneo tofauti hususani ikiwa mijini lakini kampuni ya MPOAFRIKA inataka kutofautisha dhama hiyo na kuusambaza mjini na vijijini, watoto, vijana ,na wazee wamekuwa wakilipa fedha kwa ajili ya mchezi huo unaokuja kwa kasi sasa na ambao umeshaanzishwa mashindano.
.
Mkurugenzi wa The pool table village Emmanuel Mwakabana amesema katika kuondoa dhana ya kwamba mchezo huo ni wa walevi klabu yao imekuwa ikiwahusisha watu wa rika zote na mataka mbalimbali wengine hawajawai onja pombe kabisa hata siku moja. kwanza klabu yetu hatuna huduma ya pombe tunauza soda ,juice, maji kuonyesha ni vipi mchezo wa pool hauna uhusiano na pombe ni mchezo kama ilivyo mingine kama kandanda, basketball nk. ‘pia tunataka kuionyesha jamii ya kitanzania kuwa pool sio lazima uchezwe katika bar la hasha ndio maana tukatengeneza sehemu hii nzui yenye hadhi ili kumfanya hata Yule asiyetumia kilevi kucheza mchezo huo.
.
Mwakabana anasema mbali na kuanzisha klabu hiyo iliopo eneo la Tandika Davis corner matarajio yao ni kuanzisha klabu za mchezo huo katikka kila wilaya jijini Dar es salaam na baadae Tanzania nzima ‘tumeanzisha kijiji hiki kwa lengo la kuwasaidia vijana wenzetu kuondokana na vijana wengi kujihusisha na mambo ya kijangili, ukabaji, utumiaji madawa ya kulevya, hasa ukiingia ndani ya kijiji hicho utapata raha duniani baada ya kukutana na viyoyozi, Tv bapa, saloon ya kiume ya kisasa pamoja na STUDIO ya kurekodi wasanii mbalimbali. Vitu vyote vimelifanya jengo hilo kuwa la aina yake na kuwashangaza watu wengi waliokuwa hawajui maana yake, na pia lengo jengine ni kuvumbua vipaji zaidi na kuufanya mchezo wa pool kuwa wa kimataifa zaidi na kuwa unachezwa na jinsia zote alisema Emmanuel Mwakaba.
No comments:
Post a Comment