Welcome to pwaniraha blog please contribute by posting your comments on our blog, kindly note that abussive language is strictly not entertained. Thank you.
Welcome To Pwani Raha Blog; email us at "pwaniraha@gmail.com"

May 26, 2010

Mpendazoe Aunguruma, Atoa Wiki Moja Kwa Msajili Wa Vyama.



Msemaji wa Chama cha Jamii cha CCJ Fredy Mpendazoe akitoa tamko la chama cha CCJ leo katika ukumbi wa Habari MAELEZO kuhusu kauli za msajili wa Vyama Vya Siasa Nchini John Tendwa kuhusiana na kutaka kutoa usajili wa kudumu wa chama cha CCJ Mpendazoe ametoa muda wa wiki moja kwa msajili awe amesha toa maamuzi ya kukipa chama hicho usajili wa kudumu (kulia) Mwenyeikiti wa Chama hicho Richard Kiyabo.


Mpendazoe akisisitiza jambo kuhusiana na Msajili wa vyama vya siasa John Tendwa kukataa kukipa usajili wa kudumu chama cha CCJ wakati alipokuwa akiongea na wandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO leo saa 5 Asubuhi.



Kutoka kushoto ni Msemaji wa chama cha CCJ Fredy Mpendazoe , Mwenyeikiti wa chama hicho Richard Kiyabo, Katibu Mkuu wa CCJ Renatus Muabhi ,Naibu Katibu Mkuu Dickson Ng'hily ,Katibu Mwenezi Costantina Akitanda na Afisa mwandamizi wa idara ya Habari MAELEZO Sise, wakiwa katika mkutano na wandishi wa habari leo.

Mwenyekiti wa CCJ. Richard Kiyabo.

No comments: