UVCCM ATANGAZA KUMVAA LUKUVI-JIMBO LA ISIMANI
Na mwanablog wetu Dar
MSOMI wa Shahada ya Sayansi Siasa, Jamii na Utawala ya Chuo Kikuu Dar Es Salaam na Mwenyekiti wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM)Kata ya Kimara, Felix Mdesa(33) ametangaza nia yake ya kugombea Ubunge katika jimbo la Isimani linaloshikiliwa na Wiliam Lukuvi.
Akitangaza nia yake hiyo jana jijini Dar es Salaam, Mdesa alisema kujitosa katika jimbo hilo ni kuhakikisha maendeleo yakiongezeka kwa kasi na kutoa fursa za kiuchumi kwa wananchi wa jimbo hilo.
“Mbunge anayeshikiria jimbo hilo ameweza kufanya mambo mengi mazuri, hivyo kwa kidemokrasia na kuwa na Haki ya msingi kikatiba, nitahakikisha naendeleza mambo ya msingi ambayo bado hajayatekeleza, hii ni pamoja na kuongeza nguvu kwa wananchi wengi waliokosa fursa mbalimbali” alisema Mdesa.
Mdesa ambaye kwa sasa ni mwajiriwa wa Malawi Cargo Centre (MCC LTD) na mzaliwa wa Kata ya Kihesa iliyopo ndani ya Jimbo hilo la Isimani, alisema kuwa, aamesukumwa na vitu vingi sana ambavyo mpaka sasa bado havijatekelezwa likiwemo swala Ujenzi wa lami kwa zaidi ya miaka 30.
“Nia yangu ni kuona maendeleo ya jimbo hilo yakiongezeka, hikiwemo na wananchi ambao asilimia kubwa ni wakulima wakipata fursa za kusafirisha mazao yao nje ya jimbo hilo huku vijana nao wakipata kuwezeshwa, uongozi ni kupokezana kijiti hivyo kijiti hicho nitakiongoza vizuri na naomba wananchi siku itakapofika ni kutekeleza wajibu” alisema Mdesa.
Kwa kujitokeza huko kunafanya idadi ya wagombea kufikia wawili akiwemo Mbunge wa jimbo hilo, Wiliam Lukuvi ambaye bado ameonyesha nia ya kuendelea kuliongoza.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam William Lukuvi akiwa katika semina ya wanachama wa CCM katika ukumbi wa Mliamani City,ambaye amevamiwa na Msomi wa Shahada ya Sayansi Siasa, Jamii na Utawala ya Chuo Kikuu Dar Es Salaam na Mwenyekiti wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Kata ya Kimara, Felix Mdesa(33) ametangaza nia yake ya kugombea Ubunge katika jimbo Isimani, nia ya kijana huyo kugombea jimbo hilo ni kutaka kuleta mapinduzi na kuweza kuwatumika wananchi wa jimbo hilo tofauti na Lukuvi ambaye kwa sasa amekluwa akitumikia zaidi wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam, alisema Felix.
No comments:
Post a Comment