Welcome to pwaniraha blog please contribute by posting your comments on our blog, kindly note that abussive language is strictly not entertained. Thank you.
Welcome To Pwani Raha Blog; email us at "pwaniraha@gmail.com"

April 6, 2010

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Yakoa Semina.

Mmoja wa wanasemina ambaye ni mchora katuni katika gazeti la The Citizen Kingi Kinya akichora katuni wakati alipokuwa katika semina iliyoandaliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, semina hiyo iliwalenga wachorakatuni katika magazeti nawapigapicha za habari hapa nchini katika semina iliyofanyika ukumbi wa Baraza la Maaskofu Tanzania.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Emmanuel Huba kulia akielezea shughuli za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wakati alipokuwa akihojiwa na wandishi wa habari katika viwanja vya Baraza la Maaskofu kurasini wakati wa semina ya wachora katuni za habari na wapiga picha za habari nchini.

Baadhi ya wapiga picha za habarihapa nchini wakifuatilia semina katika ukumbi wa mikutano wa baraza la Maaskofu Tanzania Kurasini,wakwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Wapiga Picha za Habari nchini PPAT Mroki Mroki na Yusuph Badi ambao wote wanafanya kazi katikagazeti la Habari Leo,wengine ni Selemani Mpochi wa The Guardian,Mhariri Mkuu wa Gazeti la Majira Emmanuel Kwitema, wakiwa katika semina hiyo.

Mkuu wa Elimu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Rahani Athumani akionyesha moja ya Katuni kwa washiriki wa semina ikiwa ni moja ya mada yake katuni hiyo ilizochorwa kwa niaba ya mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ikiwa ni sehemu moja wapo ya kutoa elimu kwa wananchi.

Makamu mwenyekiti wa Chama cha wapiga picha za Habari Tanzania, (PPAT) John Badi ambaye ni mpiga picha wa Magazeti ya Kulikoni na This Day na Fransic Dande ambaye ni mpiga picha za habari katika magazeti ya Tanzania Daima na Sayari wakifuatilia semina hiyo kwa makini .

No comments: