Pichani ni kuku wa rangi nyeusi akiwa katika maeneo ya chuo cha madaktari Muhimbili akiwa amevishwa hirizi nyeusi, nyekundu na nyeupe ,sakata hilo la kuku huyo lilitokea majira ya mchana ambapo moja ya walinzi katika eneo hilo la chuo alimuona akiwa katika moja ya madarasa bila wasiwasi wowote wala kuku huyo alikuwa haogopi mtu yeyete kiasi cha kuwafanya walinzi wa eneo hilo wajiulize mara mbili kulikoni.
kuku huyo akiwa eneo la mlango katika moja ya majengo ya eneo la hospitali ya taifa ya Muhimbili.
akiwa katika matembezi yake eneo la bustani iliyopo mbele ya geti la kuingilia kama unaungia katika chuo cha Muhimbili.
Hapa ni miondoko ya kuku huyo hirizi ikininginia shingoni. Walinzi walishindwa hata kumgusa walikuwa wakimwangalia.
No comments:
Post a Comment