Welcome to pwaniraha blog please contribute by posting your comments on our blog, kindly note that abussive language is strictly not entertained. Thank you.
Welcome To Pwani Raha Blog; email us at "pwaniraha@gmail.com"

March 6, 2010

Chama Cha Wapigapicha Habari Tanzania ( PPAT) Chapata Viongozi Wapya.

Wasimamizi wa kura wakihesabu kura zilizopigwa katika uchuguzi mkuu wa viongozi wa chama cha Wapiga picha za habari Tanzania PPAT( PRESS PHOTOGRAPHERS OF TANZANIA) kutoka kushoto Moshi Kiyungi, Mwanakombo Juma, uchanguzi huu ulifanyika katika ukumbi wa Idara Habari MAELEZO Tarehe 6 machi 2010.
Baadhi ya wanachama wakiwa wamemnyanyua mwenyekiti mpya aliyechaguliwa Mwanzo Milinga kwa kura 13 baada ya kumshinda Mroki Mroki ambaye alipata kula 6. Kutoka kulia ni Mwanakombo Juma, John Badi, Emmanuel Hermani, Benard Rwebangira na Moshi Kiyungi. Milinga amechukua nafasi ya Juma Dihure ambaye amestaafu wadhifa huo.

Mwenyekiti wa chama cha wapiga picha za habari PPAT Mwanzo Milinga aliyevaa tisheti nyekundu akimpongeza Leah Samike ambaye alishinda kiti cha uweka hazina kwa kujikusanyia kura zote Leah hapo awali ndiye aliyekuwa katika nafasi hiyo, kulia ni mpiga picha wa gazeti la The Gurdian Khalfani Said na kushoto ni mpiga picha wa gazeti la msema kweli.

Hii ndio kamati tendaji ya chama cha wapiga picha Tanzania (Press Photographers of Tanzania) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuchaguliwa na mkutano mkuu wa chama. Kutoka kulia Mwanakomba Juma Mweka hazina Msaidizi, Mroki Mroki Katibu Mkuu wa tatu Mwanzo Milinga Mwenyekiti wanne John Badi makamu mwenyekiti na wa tano Leah Samike katibu mkuu.