
Naibu waziri wa wizara ya Mawasiliano na Teknolojia mauwa Daftari akibidhiwa msaada wa hundi ya shilingi Milioni 2 na Afisa Mawasilano wa Vodacom Tanzania Mwamvua Mlangwa kwa ajili ya kikundi cha kina mama wa Mjini Wete. Fedha hizo ni kwa ajiri ya kukiendeleza kikundi hicho.

Naibu waziri wa wizara ya mawasiliano na Teknologia Dr Maua Daftari(katikati)akifuturu pamaja na Afisa uhusiano wa Vodacom Mwamvua Mlangwa(kushoto)Mwenyekiti wa umoja wa wanawake Tanzania(UWT)mkoani kaskazini Pemba, Sada Thaniy. Vodacom Foundation waliandaa futari hiyo kwa ajili ya watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu.

Meneja wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule(kushoto)wakifuturu pamoja na wakazi wa mjini Wetemkoani kaskazini Pemba.

Msaada huo uliambatana utoaji wa vitu mbalimbali ambavyo vilikuwa na thamaini ya shilingi milioni 2 kwa ajiri ya kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu. Ikiwa ni pamoja na kufuturisha watoto hao wa Wete Mkoani Kaskazini Pemba.

Baadhi ya watoto wa Almadrasat ya Irshadu Atfal Kamariya ya Wilaya ya Wete wakiwa katika swala kabla ya kupata futari iliyoandaliwa na Vodacom Foundation kwa watoto yatima na waishio katika mazingira magumu wilaya wete iliyopo Kaskazini Pemba.
Kukaa design hii ni ngumu sana haswa kama una kiribatambi we jaribu uone.
1 comment:
Mbano watu wazima pekee ndio wanaokula kisha watoto wote hamna kitu wengine wameshika tama. Ama ndio heshima kwenye chakula wakubwa wamalize ndio wadogo wapate fursa.
Post a Comment