Welcome to pwaniraha blog please contribute by posting your comments on our blog, kindly note that abussive language is strictly not entertained. Thank you.
Welcome To Pwani Raha Blog; email us at "pwaniraha@gmail.com"

August 13, 2009

Hospitali ya Ludewa

Mfanyabiashara ya Dagaa wa ziwa Nyasa katika soko kuu la Songea Ruvuma Editha Kiwila akipanga bidhaa yake ambao kisado kimoja huaza shilingi 2000 hadi 4000.(Picha na Albart Jackson.)

Akina mama ambao wanawauguza ndugu zao katika hosptali ya Wilaya ya Ludewe wakisonga Ugali nje ya wodi ya akina mama wanaosubiri kujifungua,kati ya akina mama 100,000.wajawaito 200 hupoteza maisha katika Wilaya hiyo kutokana na ukosekanaji wa miundombinu. (Picha na Albart Jackson)

Wanawake wajawazito toka katika vijiji 76 vinavyo zunguka Wilaya ya Ludewa wakiwa wamelala na wengine wakila chakula huku wakiwa wamesubilia siku zao za kujifungua katika hospitali ya Wilaya ya Ludewa Mkoa wa Iringa kati ya akina mama 100,000 wajawazito 200 hufariki kutokana na ukosefu wa huduma.


Inasikitisha: Baadhi ya akina mama wajawazito wakiwa nje ya wodi ya wazazi katika hospitali ya Wilaya ya Ludewa ambapo jengo hilo lina vitanda 6 na kila kitanda hutumiwa na akina mama wajawazito wawili. Wengine hulazimika kulala chini.

5 comments:

Simon Kitururu said...

:-(

Anonymous said...

yani hii ndio hospitali?

Anonymous said...

kama hii ndo hospitali ya wilaya, hatujafika bado safari ni ndefu.

John Mwaipopo said...

Ndugu yangu tuache utani, this cant be a district hospital, despite our country being poor. mbona za wilaya'zao' nzuri tu.

Hata hivyo picha ya juu inantoa udenda nawapenda sana dagaa wa nyasa hunambii. asiyewahi kuwala hajui

Anonymous said...

hii picha ya mwisho ni potofu mzee wa pwani....usahihi ni kuwa jengo hili ndilo uliloita waiting home si kweli kuwa ni wodi ya wazazi.hapa wanakaa kusubiri siku ya ujio wa mtoto na ni kam mita 200 toka ilipo hospitali sahii na hii nyumba ilibangishwa na serikali ilim kuondoa adha kwa wakazi wa mji wa ludewa ambao walikuwa na kazi ya kupokea mama wajawazito kutoa vijijini wakisubiri kujifungua,sisi wenye ndugu kadjhaa ilikuwa kila baada ya wiki mbili unapokea mgeni au wageni wa aina hiyo hivyo duu ilihitaji uvumilivu,lakini baada ya hii nyumba kidogo tumesaidiwa hatupeani lawama tena.......mdau mkubwa wa ludewa na vitongoji vyake