Welcome to pwaniraha blog please contribute by posting your comments on our blog, kindly note that abussive language is strictly not entertained. Thank you.
Welcome To Pwani Raha Blog; email us at "pwaniraha@gmail.com"

August 13, 2009

Kulipa Kodi ya Mwaka Mzima ni Poa au Kunaumiza?

Gazeti la Uhuru linaendelea hivi
Wanaotumia fedha za umma kulipia pongo. "licha ya kwamba za Dar es salaam na kwengineko nchini hazina hadhi ya kulinda haki ya mtu kuishi katika mazingira safi salama, si halali kisheria kwa mwenye nyumba kutoza kodi kwa kipindi zaidi ya mwezi mmoja kwa mara moja, tena kabla ya mpangaji hajakaa kwenye nyumba. Soma zaidi......

"Ni kosa kubwa kumlazimisha mtu alipe kodi ya mwaka, hana uwezo au fedha hizo. Sheria tunayo tatizo hatuna watekelezaji hizi sheria," alisema Kahangwa. (mwisho wa kunakili gazeti)
Pwani Raha limegundua kuwa watu (hususana vijana) wanaoanza maisha inakuwa vigumu sana kumudu gharama halisi za kuishi. Utakuta mtu anapoanza kazi analipwa mshahara pengine Tsh 300,000 kwa mwezi. Kodi ya nyumba ni Tsh 75,000 kwa mwezi ila anatakiwa alipe Tsh 900,000 ambayo ni kodi ya mwaka (hapo fee ya dalali hatuja hesabu). Vijana wengi hukopa ili waweze kumudu gharama halisi. Wengine hukopa mikopo ambayo marejesho ni ya miaka mitatu kisha akalipa kodi ya mwaka wa kwanza. Mwaka unapomalizika kijana husika hukwama maana mkopo haujafikia hata nusu na anatakiwa alipekodi ya mwaka mzima tena. Hali hii huchangia watu kujihusisha na mbinu mbadala za kujipatia fedha, ambazo mbinu nyengine huwa kinyume na sheria.

Source: Gazeti la Uhuru (Agosti 3,2009)

No comments: