Welcome to pwaniraha blog please contribute by posting your comments on our blog, kindly note that abussive language is strictly not entertained. Thank you.
Welcome To Pwani Raha Blog; email us at "pwaniraha@gmail.com"

July 22, 2009

Vodacom Wakopa USD 90M kutoka CITIBank.

Kushoto ni mkurugenzi mkuu wa Vodacom Bw. Dietlof More pamoja na mkurugenzi mkuu wa Citibank Bw. Noveed Riaz wakitia sahihi kwenye mkataba.


Kampuni ya simu za mkononi ya vodacom imekopa dola za kimarekani milioni 90 kutoka kwa benki ya Citibank kwa lengo la kuimarisha mtaji wake. Citibank inatoa huduma ya mkopo ndani ya miaka mitano wenye thamana ya dola za kimarekeni milioni 150 ambapo dola milioni 90 zilizotolewa zimepatikana hapa hapa nchini, fedha zilizobaki zitapatikana nje ya nchi. Akizungumza wakati wa hafla ya fupi iliyofanyika katika ofisi za Vodacom zilizopo katika jengo la PPF Mkurugenmzi Mkuu wa Vodacom Dietlof Mare aliipongeza banki hiyo kwa uamuzi wake wa kutoa mkopo huo ambao utawawezesha kuendeleza huduma mbalimbali katika jamii ya Watanzania. (Soma zaidi/Read more....)

Naye Mkurugenzi wa Fedha wa Vodacom Christopher Fawcett alisema kupatikana kwa fedha nje ya nchi kusingewezekana bila ya juhudi za benki za ndani ya nchi hivyo wanajivunia uhusiano wao na benki ya Citi kwa kuwa mstari wa mbele kusaidia katika maswala mbalimbali ya kijamii nchini Tanzania. Kwa upande wake Ofisa Mkuu wa Citibank kitengo cha ukanda wa Afrika Noveed Riaz alisema sababu kubwa ya ushirikiano wetu katika ufanisi wa mkopo huo ni imani kubwa waliyonayo kwa kampuni ya vodacom kwa upande wa vodacom Mkurugezi Mkuu Dietlof More na Christopher Fawcet walishukuru benki hiyo kwa kuwa na mipanga ya kusaidia jamii hasa kupitia mkopo huo.

Vodacom imekuwa ikijihusisha na kutoa misaada mbalimbali katika jamii ya Tanzania Ambapo kitengo cha Vodacom Foundation kimekuwa katika harakati za kuhakikisha shule zinajengwa na kutoa misaada ya madawati katika mikoa yote ya Tanzania ambapo kwa kipindi hiki Vodacom Foundation wametoa misaada ya madawati 400 katika baadhi ya shule za jijini Dar es salaam. sehemu nyingine ambayo watanzania wanajivunia kutoka kwa vodacom ni udhamini wa mpira wa miguu ambapo vodacom imedhamini ligi ya Tanzania bara ambayo inajulikana kwa jina la Ligi kuu la Vodacom Tanzania bara.

Kingine ni udhamini wa shindano la Miss Tanzania ambapo kwa mwaka huu wametenga zaidi ya shilingi Milioni 600 kwa ajili ya kufanikisha shindano hilo kuanzia vitongoji hadi kimataifa.

No comments: