Mshiriki wa shindano la Miss Temeke Sarah Steven ambaye ni miongoni mwa washiriki 12 wanaowania nafasi yakuwa kimwana wa Temeke amejigamba kuwa kutokana jinsi alivyojiandaa katika shindano hilo, atautwa ubingwa. Mrembo huyo aliyeshinda taji la kuwa mrembo wa Gazeti la The football linalomilikiwa na Kampuni ya Lady band inachapisha magazeti ya Changamoto na the Football. Pia mrembo huyo alifanikiwa kuingia makataba wa kazi wa miaka miwili akiwa kama meneja masako, Sarah alizaliwa mkoani Arusha miaka 21 iliyopita na kupata elimu ya msingi katika shule ya msingi ya Naura iliyopo Arusha mwaka 2002 alijiunga na Sekondari ya Usiniver ya Arusha hadi mwaka 2005 ambapo alihitimu elimu yake ya kidato cha Nne, Mwaka 2006 na 2007 alijiunga katika shule ya Green Bird Girls High School ya Kilimanjaro, ambapo alihitimu kidoto cha sita mwaka 2007 mwezi wa tisa anategenma kujiaunga na chuo cha Ushirika Moshi kwa masomo ya uhasibu. Akizungumzia ushiriki wake katika shindano la Miss Temeke amesema kuwa ni faraja kwake na anamini kuwa atashinda.
July 29, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
please shave makwapa!
Post a Comment