Mashine ya kutengeneza Kondomu ambayo kwa afrika mashariki ni moja tu na ipo hapa Tanzania TBS.

Unaona hapa; hauhitaji komputa zenye 'flat screen" kufanya kazi bora. Hata printer ni ya kawaida kabisa sio heavy duty, hani ukiprint page kumi inachukuwa dakika kumi.

Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Charles Ekelege akikabidhiwa cheti cha umahiri na Meneja Maabara wa Kampuni ya Sanas ya Afrika Kusini Marlan Pillay katika hafla iliyofanyika katika ofisi za TBS jana ambapo maabara ya kemia na Maabara ya Kondom zilitunukiwa vyeti vya Umahiri.

Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wakiwa katika hafla ya kushuhudia upokeaji wa vyeti kwa Umahiri wa maabara za TBS kutoka kwa kampuni ya SANAS ya Afrika Kusini ambapo maabara ya Kondomu na Maabara ya Kemia zimetunukiwa vyeti vya ubora. TBS ina jumla ya vyeti vinne, cha kwanza Maabara ya ugezi ilipata umahiri mwaka 2007.
Maabara ya chakula Microbiolojia ilipata cheti cha umahiri mwaka 2007, maabara ya kemia April 7 2009 na maabara ya Kondomu 1 june 2009,
No comments:
Post a Comment