
Leo mambo yalikuwa kama hivyo hapa Dar, mvua imenyesha sana, na kulingana na miundombinu mibovu basi maji yalijaa kwenye barabara mpaka Posta hali ilikuwa si shwari.

Ukitaka uvuka barabara sharti uvue viatu.

Hawa ndio nguvu kazi, hapa wanajinadi. Kila mmoja anasema kuwa yeye ana nguvu ya kubeba mtu. Shughuli yao kubwa hapa ni kubeba watu ambao hawataki kuvua viatu.

Sijui huyu dada tumuite abiria au mteja, mambo ndio kama hivyo unavyoona.
 
 
1 comment:
Jamani, mwaka huu na miji mikuu Afrika yafurika hivi kwa mvua kidogo vile? El-Nino ikirudi tutafanya nini? Viongozi wetu wafaa kushughulikia haya mambo
Post a Comment