Mwanamuziki aliyewahi kuvuma miaka ya tisini Kanda Bongman alishindwa kutokea katika onyesho alipangiwa kulifanya hapa nchini Tanzania. Mwanamuziki huyo ambaye alikuwa tayari ameingia mkataba na King Dodo ambaye ni maarufu kwa kuwaleta wanamuziki wa dansi kutoka Jamuhuri ya Congo. Kanda Bongoman alishindwa kutokea kabisa licha ya hivyo pia hakufika nchini. Kiongozi wa Bendi ya FM Academia ambaye alikuwa amelipwa ili kumsindikiza Kanda Bongoman alisema kuwa muandaaji wa onyesho hilo King Dodo alikuwa tayari ameshawalipa kila kitu ikiwa ni pamoja na kuandikiana mikataba lakini hadi sasa hatujui ni sababu zipi zilizomfanya mwanamuziki huyo kutotokea.
.
Hatahivyo FM waliendelea kuonyesha shoo nzuri huku vyombo vyao vikikoroma kiasi cha watu kuanza kutilia shaka maandalizi ya onyesho hilo. Kutokana na wabongo kupenda starehe waliendelea kulipa kingilio cha 5000, kwa ajili ya kuwaona FM ACADEMIA. THT Tanzania House of Talent walishindwa ku-perform kutokana na deki yao ya muziki kushindwa kusoma CD.
No comments:
Post a Comment