Magufuli aliwapongeza askari wa Tanzania na wale wa Afrika Kusini kwa kuwazawadia vitu mbalimbali. Oparesheni hiyo ilifanywa na meli ya Sahar baartman ya Afrika kusini baada ya kukodiwa na Wizara ya Uvuvi na Mifugo kwa ajili ya kukomesha wizi wa samaki unaofanywa na mataifa matajiri duniani. Kwa muda wa miaka hamsini haikuwahi mkukamatwa kwa meli yoyote pamoja na kuwa tayari Tanzania ina rada ya kuweza kuona uhalifu baharini, lakini ilikuwa inashidwa namna ya kuweza kupata vifaa vya kuweza kuwafikia maharamia hao. Rais Jakaya Kikwete amewapongeza mashujaa hao waliofanikiwa kukamtwa kwa wahalifu hao, pia ametoa onyo kali kwa maharamia hao na kubainisha kuwa nchi ya Tanzania, Kenya, Msumbiji hazitakubali kuona vitendo hivyo vinaendelea.
March 10, 2009
OPARESHENI YA MAGUFULI YAKAMATA MELI YA MAHARAMIA TOKA VIETNAM
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment