Kama kawaida yao vituko kwao havikosi kila mmoja aliingia nan gari lake huku kiongozi wao Seki akitangulia kuandaa na kuwawekasawa watu.
Mama Mabele akifanya vitu vyake.
Masanja mbele akikandamiza kibara wakati Joti akiruka kijotijoti.
Wakuvanga na manjonjo yake.
.
Kundi la maigizo la Original Comedy leo wametoa mpya wakati wa uzinduzi wa siku ya wanawake katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa Mama Salma Kikwete.Umati wa watu uliofurika hasa watoto wa shule za sekondari na msingi katika viwanja hivyo ulishindwa kabisa kumsikiliza kwa makini mama kikwete pale alipokuwa akihutubia. Wengi wa watu wazima walisikika wakisema watoto hao wanapiga kelele kwa kutaka comedy waanze mara moja kuonyesha onyesho lao. Mc wa shughuli hiyo alisikika akiwatuliza wanafunzi hao na kuwatishia kuwa iwapo hawatakuwa na subira na utulivu basi onyesho hilo halitakuwepo.
.
Baada ya Mama Salima kumaliza hutuba yake kwa wananchi aliwaaga na kuondoka kuendelea na majukumu yake mengine ya kujenga taifa. Hapo ndipo watu wakubwa kwa watoto walianza kusukumana kila mmoja wakitafuta nafasi ya kuwaona. Kama kawaida yao vituko kwao havikosi kila mmoja aliingia na gari lake huku kiongozi wao Seki akitangulia kuandaa na kuwaweka sawa watu. akaaza "jamani eehh mnataka orijino Komedy?" Watu "ndiyooo" wazee wakazi wakaingia mmoja baada ya mwengine Mama Mabele akaingia akiwa amevaa kama mama Salma Kikwete, akafuatia wengine Wakuvanga, Joti, Mpoki, Vengu na Masanja.
No comments:
Post a Comment