

pichani ni jafaray akiwa na mwanamuziki ambaye amemshirikisha katika nyimbo yake yan Wali Nazi Fatma Kilimati.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Jafaray Mshamu ameingia studio na kufyatua nyimbo tano ambazo tayari zimeshakamilika na zimeanza
ku-hit katika vituo vya redio hapa nchi. Alizitaja kuwa ni Wali Nazi ambayo itabeba jina la albamu hiyo, Unapenda nini, Yeye na mimi, Nisijisahau, Saa nyingine na Jafaray. Nyimbo nyengine tano bado hazijakamilika ila baada ya nwezi huu albamu yenye nyimbo kumi itakuwa tayari.

Fatma Kilimati akishikilia ndizi mkononi; sijui anamaanisha nini hapa ila aliimba vizuri.
No comments:
Post a Comment