.
Mgodi wa almasi wa Williamson Diamonds Limited (WDL) ulioko Mwadui ni wa ubia kati ya kampuni ya Willcroft CompanyLimited (Kampuni tanzu ya cheviotHoldingsLimited)inayomilikiwa na kampuni kongwe ya Almasi duniani- De Beers ya Afrika kusini yenye hisa 75% na serikali ya Tanzania yenye hisa 25% .
.
Mgodi wa WDL umekuwa ukiendeshwa kwa hasara kwa takribani miaka 15 iliyopita. Serikali kwa kushirikiana na De Beers wamekuwa wakifanya juhudi nyingi kuufanya mgodi wa WDL uzalishe kwa faida ikiwa ni pamoja na kuiajiri kampuni ya Ukaguzi wa mahesabu na ushauri wa Biashara ya KPMG ya Afrika Kusini mwaka 2004 kutathmini hali ya uendeshaji na kifedha ya WDL (operational and financial issue facing WDL). Lengo lilikuwa kuishauri serikali hatua ya kuichukua kutokana na mwenendo wa kiuzalishaji na kifedha wa mgodi huo kuendelea kuwa mbaya tangu 1994 serikali ilipouza hisa zake 25% kati ya 50% ilizokuwa nazo kabla ya oktoba 19, 1994 na pia kufanyika uwekezaji mpya wa Takribani Dola za Marekani millioni 18.
.
KPMG iliishauri serikali ifanye uamuzi kuhusu hisa zake 25%; wa ama kuziuza au kuzipunguza kwa kuchangia gharama za upanuzi wa mgodi uliokuwa umependekezwa na kampuni ya De Beers. Serikali haikukubaliana na ushauri huo kwa sababu mapendekezo ya KPMG kwa wakati huo yangeinufaisha zaidi kampuni ya De Beers.
















No comments:
Post a Comment