
Habari zilizotufikia sasa hivi ambazo niza kuhuzunisha zinaeleza kuwa Katibu mwenezi wa Yanga Francis Lukas amefariki Dunia kweli nijambo limetusitua sana hasa wapendamichezo hususni Klabu ya Yanga , MENGI aliyafanya wakati akiwa kiongozi wa Yanga ilikuwa ni pamoja na Kulifufua gazeti la Yanga ambalo kwa hakika lilishika vilivyo hapa jijini na mikoa yote ya Dar es Salaam. Francis kwa mara ya mwisho kumwona kwa macho yangu ilikuwa katika mechi ya kuwania ubingwa wa Afrika katika mechi ya Comoro na Yanga iliyopigwa uwanja wa Zamani wa Taifa mnamo tarehe 31 January, toka hapo tena sikubahatika kuonana naye hadi leo nitulipoambiwa AMEFARIKI.Francis alikuwa mchapa kazi hasa kitengo cha Upigaji mpicha za habari hasa za michezo. Jamani tumuombee tatutangulia nasi tuko nyuma.
Hizi picha nilibahatika kumpiga marehemu Francis Lucas uwanja wa Taifa katika mechi ya Yanga na Comoro akiwa amekaa katika benchi la ufundi.
Na Mpiga picha wetu
No comments:
Post a Comment