


Tamasha la kubwa la reggae la kuukaribisha mwaka mpya wa 2009 na kuuaga mwaka 2008 litafanyika leo jioni katika ukumbi wa Kilimanjaro 2000 uliopo Mwenge Dar es Salaam. Tamasha hilo limeandaliwa na Chama cha Marasta hapa nchini Tanzania TARAMO, pamoja na onyesho hilo kutakuwepo na burudani nyingine ambazo zitaambatana na muziki wa Disko ikiwa ni moja ya kusherehekea mwaka mpya. Muziki wa Reggae utapigwa live .
Ras Bumija na Ras Gwandumi walimwambia mwandishi wa Pwani Raha kuwa tamasha hilo limeandaliwa ili kuwakusanya pamoja wapenzi wa muziki wa Raggae kutoka pembe zote za Jiji la Dar se Salaam na vitongiji vyake, ilikuukaribisha mwaka mpya kwa burudani zaidi. Bendi ya Machifu itatoa burudani ikiwa chini ya MADJ wazoefu wakiongozwa na DJ machachali Jah Bleze na Badi Sungu, patakuwa hapatoshgi watu wote mnakaribishwa kujione watu wenye Dread Locks za kuvutia majaa wa kweli wenye amani na upendo.
Burudani itaanza saa 2 usiku hadi majogooo. ukumbi upo Mwenge karibu na kituo cha mabasi mwanzoni kabisa kama unatokea Posta (KILIMANJARO 2000).
No comments:
Post a Comment