Wasanii wa kundi la Warriors lenye maskani yake pale Msasani jijini Dar es Salaam wakionyesha umahiri wao katika moja ya maonyesho yao. Kundi hili lenye wasanii zaidi ya 30 lilianza kama masihara baada ya kujikusanya katika mtaa wa Mandazi road likiwa ni kundi la kushangilia timu ya Kambarage ya Msasani ambayo enzi hizo ikiuwa daraja la tatu wilaya ya Kinondoni. Baada ya hapo walipata nafasi ya kufanya mazoezi katika ukumbi wa New Msasani Club kama wacheza shoo hapo ndipo vipaji vilianza kuonekana, wasanii wakubwa wenye majina walianza kuwakodi ili wawatumie wakati wanapofanya shooting za video. Si hapo tu, kwa sasa makampuni mengi ya kibiashara yamekuwa ya kiwatumia katika matangazo, hivi majuzimtu kampuni ya bia ya TBL kupitia kinywaji chake cha Tusker waliwakodi katika mashindano ya kombe la Tusker lililozishirikisha timu za hapa nchini, Uganda na Kenya.
Akiongea na mwandishi wa habari hii mmoja wa waneguaji mahiri Mwanaisha Seif, alisema kuwa kwa hivi sasa wamekuwa wakijipatia kipato kupitia unenguaji hivyo wameweza kuepukana na swala la utegemezi. Anaongeza kusema kuwa kazi hii inahitaji uvumilivu kwani wanume wamekuwa wakiwasumbua sana hasa kutokana na uchezaji wao lakini wamekuwa makini sana na swala hilo na kuwaasa wasichana wenzao wasichague kazi.
No comments:
Post a Comment