Kumbe George Bush yuko njema, angalia jinsi alivyokwepa kiatu alichorushiwa na mwandishi wa habari wa televisheni ya Baghdadia aliyechukizwa na ujio wa rais Bush. Bw Muntadar Al-Zeidi alirusha viatu hivyo huku akimtukana Bush kwa maneno haya"Hili ni busu la kwaheri wewe mbwa!", kwa kimombo ni "This is your farewell kiss, you dog!" akaongeza maneno haya "This is from the widows, the orphans and those who were killed in Iraq." akimaanisha " Hii nikutoka kwa wajane, yatima na wale waliuwawa Iraq". Tukio hilo lilitokea jana baada ya rais Bush kufanya ziara ya siri huko Iraq kwa maongezi kuhusu vita vya Iraq.
Hapa raisi bush anaonekana akipwepa kiatu cha pili, inaonekana Al-Zeidi alipomkosa na kiatu cha kwanza akajaribu kishusha urefu iliampate vizuri lakini Bush naye alizama zaidi.
Bush akiongea baada ya kurishiwa viatu, akatania kuwa viatu hivyo vilikuwa saizi kumi (size 10). Sasa walinzi wa Bush wanamlinda kwa karibu sana kama unanyoona kwenye picha.
Raia wa Iraq akisherekea jinsi raisi Bush wa Marekani alivyorushiwa kiatu. Inasemekana kwa tamaduni za Wairaqi kuwa kumrushia mtu kiatu ni ishara ya mshusha hadhi au kumtushi mtu (insult). Tukirudi nyuma mwaka 2003 wakati sanamu la Saddam Hussein lilipoangushwa na wananchi wake, watu hao walilipiga sanamu hilo kwa kitumia viatu kuashiria jinsi walivyomshusha hadhi Saddam.
No comments:
Post a Comment