Jana kulikuwepo na ajali mbaya maeneo kati ya taa ( traffic lights) za Morocco na Fao Jijini Dar es salaam, ilikuwa kama saa tano za usiku. Ajali hiyo ilihusisha gari ndogo aina ya Toyota Cresta GX 90 (balloon) yenye namba za usajili T180 AQA na Daladada aina ya Toyota Coster yenye namba ya usajili T146 AKC inayomilikiwa na Ibrahim M Shayo kwa mujibu wa maandishi yaliyopo chini ya mlango wa dereva. Kulingana na shuhuda aliyetambulika kwa jina moja Bw Juma, gari hilo dogo lilitaka kuingia upande wa daladala (overtake) kwa ghafla huku daladala hiyo yenye abiria ikiwa kwenye mwendo wa kasi.
Hapo juu picha inaonyesha kuwa gari halikuwa private maana kibao kinaonyesha neno PRIVATE linaelekea ndani ya gari. Ni wazi kuwa gari hili ni la Mabibo na eneo la ajali ni barabara ya Ali Hassan Mwinyi, sasa gari hili lilikuwa linafanya biashara gani huku. Nashauri mamlaka husika zichukue hatua kali ili iwefunzo kwa daladala zenye tabia hii ya kuiba ruti.
Gari hili dogo lilibanwa kwenye mti wa umeme na daladala lakini cha ajabu mti huwo ulisimama imara. Hongera TANESCO kwa kuweka miti imara, bila hivyo kungekuwa na maafa zaidi.
Gari hili dogo lilibanwa kwenye mti wa umeme na daladala lakini cha ajabu mti huwo ulisimama imara. Hongera TANESCO kwa kuweka miti imara, bila hivyo kungekuwa na maafa zaidi.
Kiti cha mbele cha abiria kikiwa na damu hii inaashiri kuwa abiria huyo aliumia kiasi cha kuvuja damu.
No comments:
Post a Comment