Shindano la kumtatafuta mrembo wa kanda ya Ilala mwaka huu litajulikana kuwa ni Redds Miss Ilala 2010 na litashirikisha warembo 18 ambao wametoka kwenye vitongoji mbalimbali vilivyoko katika Manispaa ya Ilala.
Warembo walianza mazoezi wiki moja iliyopita hapa katika Hotel Apartment ya Ramada chini ya waalimu wanne ambao ni Star anayefundisha kucheza na kulitawala jukwaa. Leila Bhanji anawafundisha kutembea, kujiamini na kujitunza. Kamati hiyo pia imekuwa ikikaribisha wataalamu wa mambo mbali mbali kuja kuwasaidia washiriki ili wawe tayari kimwili na kisaikolojia kwa ajili ya shindano la Redds Miss Ilala 2010 litakalo fanyika Ubungo Plaza tarehe 26 Juni. Ruge Mutahaba pia naye alikuwepo kusaidia kutoa somo kuhusu vipaji na namna ya kujitambua na kukuza vipaji. Leo tutakuwa na maafisa wa Manispaa ya Ilala ambao wataendesha mafunzo mbali mbali ya uzalendo kwa warembo ili waijue Manispaa yao, mkoa wao na nchi yao nzuri ya Tanzania. Mashindano ya mwaka huu ya kumtafuta Mrembo atakaye beba bendera ya Manispaa ya Ilala yatakuwa tofauti na mashindano tuliyozoea. Kuna vipengele ambavyo waandaji wamevibuni na kuviongeza ili kunogesha shindano hilo na kulifanya libaki katika kumbukumbu ya mashindano bora yaliyowahi kufanyika hapa Tanzania. Shindano la Redds Miss Ilala 2010 limedhaminiwa na Taasisi kadhaa ambazo ni vyema tukazitambua na kuzishukuru kwa kuendelea kutoa ushirikiano wa kuendeleza sanaa hii ya urembo.
1. Redds Premium Original ambao ndio wadhamini wakuu wa shindano hili, ambao ndio wanaotuwezesha kuboresha na kutoa Zawadi tutakazo zitangaza baadaye.
2. Vodacom Tanzania ambao ni wadhamini wakuu wa shindano la Miss Tanzania.
3. Lamada Hotel Apartment ambao ndio wanaotutunza na kutupatia sehemu ya kuishi na kufanyia mazoezi na shughuli mbalimbali.
4. Aurora Security ambao wanatusaidia kwenye usafiri, Ulinzi na mambo mbali mbali ili warembo wajisikie kuwa salama na tayari kwa mashindano.
5. Muzasha Tours and Safaris kwa kusaidia kufanikisha kambi
6. Sofia Production atakao fanya production ya Event
7. SYSCORP Group ambao wataweka billboards na Street banners
8. Valye Spring Watakao tengeneza jukaa na kufanya Decorations
9. Primetime Promotions watakaoshughulikia Sound System
10. Fabak Fashion watakao wavalisha warembo na kuwapendezesha
11. CXC Africa ambao wanasaidia mambo mbali mbali kuwezesha shindao liwe la hadhi
12. Africa Media Group kupie channel ten na Magic FM kutangaza na ku promote shindano
13. Clouds FM ambao watatangaza na ku promote shindano
14. Habari leo, Gazeti la Serikali watakao tangaza na ku promote Shindano
15. Jambo leo ambao wata promote shindano
Warembo walioko kwenye kambi ya Redds Miss Ilala 2010 ni 18 kusimamiwa na Sylivia Shally ambaye ni Miss Ilala anayemaliza muda wake. Warembo hao ni Salma Mwakalukwa, Doreen Mutabingwa, Sarah Nalolah, Joyce Sadick, Lilian Massam, Cynthia Bavo, Consolatha Lukosi, Ritha Swai, Happiness Mushi, Ummy Mohamed, Neema Jacob, Harrieth Mulumba, Sanza Mukajanga, Agness Francis, Mariam Kimario, Neema Allen, Bahati Chando na Celine Wangusu.
Mwaka jana kanda ya Ilala pamoja na kutokufanikiwa kushinda Taji la Miss Tanzania ilifanya vizuri sana na kuvunja rekodi mbili kwenye historia ya mashindano ya Miss Tanzania. Kwa kufanya hivyo, kampuni ya Dar Metropolitan Promotions ambayo ndiyo imekuwa ikiandaa mashindano ya Miss Ilala kwa miaka 12 sasa ikawa imejiongezea rekodi zake kwenye mashindano haya. Rekodi zilizovunjwa mwaka jana. Kwa mara ya kwanza Kanda moja iliingiza Warembo watano kwenye kinyang’anyiro cha kumtafuta Mrembo wa Tanzania. Kwa kawaida na kwa kufuata kanuni ni warembo watatu tu wanaoingia kwenye Kambi ya Miss Tanzania kutoka kila Kanda. Kwa ubora wa washiriki mwaka jana, warembo watano walichaguliwa kuiwakilisha kanda ya ilala. Warembo wanne wa Miss Ilala waliingia kwenye kumi bora ya Miss Tanzania.
No comments:
Post a Comment