Welcome to pwaniraha blog please contribute by posting your comments on our blog, kindly note that abussive language is strictly not entertained. Thank you.
Welcome To Pwani Raha Blog; email us at "pwaniraha@gmail.com"

June 17, 2010

Jamii Yatakiwa Kuwalea Watoto Vyema.

Baadhi wa watoto wakiwa katika sherehe ya siku ya mtoto wa Afrika iliyoadhimshwa jana , mfanyabiashara mashuri jijini Dar es Salaam Sarehe Bin Zoo wa pili kutoka( kulia) akiwa na watoto hao katika Hoteli ya Kunduch Beach.
.
Jana Juni 16 ilikuwa ni kilele cha maadhimisho ya mtoto wa Afrika jamii iliombwa kuwakumbuka watoto wa mitaani ambao wanaishi katika mazingira magumu ili nao waonekane kama watoto wengine.Hayo yalisema na Mfanyabiashara Salehe Bin Zoo alipokuwa akisherekea na watoto hao wa mitaani katika Hoteli ya Kunduchi Beach .Salehe Bin Zoo alisema kuwa tatizo la watoto wa mitaani ni la kila mmoja hivyo ni jukumu letu kujitokeza na kuwachangia pasipo kuchoka.Kila mmoja anapaswa kuwachangia watoto hawa wa mitaani ikiwemo huduma ya maradhi, chakula na huduma ya Afya” alisema Bin Zoo. 

Tanzania inaungana na nchi wanachama wa umoja wa Afrika kuadhimisha siku ya mtoto wa Afrika inayofanyika Juni 16 kila mwaka kukumbuka mauaji ya watoto huko Soweto Afrika kusini, kauli mbiu ya mwaka huu ni “Imarisha Familia mtoto apate haki yake.Tanzania imekuwa ikiadhimisha siku hii kwa miaka kumi na tisa (19) mfululizo tangu mwaka 1991, tofauti na miaka ya nyuma mwaka huu hakutakuwepo na maadhimisho ya kitaifa bali kila mkoa utapata fursa ya kupanga namna ya kuadhimisha siku hii. Akizungumza na waandishi wa habari Katibu mkuu wa wizara ya jamii, jinsia na watoto amesema kuwa pamoja na kukumbuka mauaji hayo ya kinyama madhumuni mengine ni wajibu wa serikali za Afrika kwa watoto, mipango ya serikali kuwaendeleza watoto na kufahamu matatizo yanayowakabili watoto. Amesema kuwa serikali hutumia siku hii kutafakari kwa kina matatizo yanayowakabili na kuyatafutia ufumbuzi, pia kupitia maadhimisho hayo serikali inapata fursa ya kutangaza sera, programu na mipango inayowahusu watoto na kuhamasisha jamii kuchangia kuondoa matatizo ya watoto kote nchni.
.
Kwa mujibu wa katibu mkuu huyo maadhimisho hayo ni sehemu ya utekelezaji wa sera zinazohusu kuwaendeleza watoto ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa mikataba mbalimbali ya kimataifa inayohusu haki na ustawi wa mtoto.Kuhusu kauli mbiu ya mwaka huu amesema lengo ni kuikumbusha familia na jamii kuwa wakati wote suala la utoaji wa haki za msingi iwe ni agenda ya kudumu, amesema kuwa familia ndio msingi mkuu katika jamii hivyo ni muhimu sana iimarishwe ili iweze kuwatunza na kuwapatia haki sawa.Haki hizi ambazo mtoto anatajiwa kuzipata ni kulindwa, kuendelezwa, kushiriki na kushirikishwa, kuishi na kutokubaguliwa.Amewakumbusha watanzania kuwa watoto ni taifa la leo na kesho hivyo wanapaswa kuendelezwa ili kuwapa fursa ya kujenga taifa watakapokuwa watu wazima. Pia ameviomba vyombo vya habari kutoa ushirikiano wa hali ya juu kuhusu umuhimi wa siku hii.

No comments: