Welcome to pwaniraha blog please contribute by posting your comments on our blog, kindly note that abussive language is strictly not entertained. Thank you.
Welcome To Pwani Raha Blog; email us at "pwaniraha@gmail.com"

June 3, 2010

AIR OMAN YAANZA TENA SAFARI ZAKE ZA TANZANIA NA OMAN

Ndege ya Shirika la Ndege la Air Oman ikiwa imeegesha katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jk Nyerere jijini Dar es Salaam, shirika hilo limezindua tene safari za Tanzania na Oman baada ya kusimama kwa muda. mpaka sasa tayari imesha anza kutoa huduma hiyo lakini Rasmi itakuwa mwezi wa Nane mwaka huu.

Mkurugenzi Mkuu wa Uhusiano wa Shirika la Ndege la Air Oman, Philippe Georgious, (katikati )akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa shirika hili baada ya kuzungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, juu ya kuanza upya kwa safari za ndege za shirika la Air Oman. kutoka kushoto ni Ngwe Phyu Zar ,Sumika Bajracharva,Somaila na Moushaki.


Mkurugenzi Mkuu wa Uhusiano wa Shirika la Ndege la Oman Air, Philippe Georgious, akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini jana juu ya kuanza upya kwa safari za ndege za shirika la Oman Air, kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa shirika hilo,Mohammed Mubarak Al- Shikely,kulia ni Ejaz Khan Meneja wa Ukanda wa Afrika na Uarabuni.
Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa Bernad Membe akisalimiana na mmoja wa viongozi wa shirika la ndege la Air Oman Salm Al Hakamani wakati walipokutana katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwali JK Nyerere jana, sehemu maalumu ya kupumzikia viuongozi VIP.
Rais wa Zanzibar Abeid Aman Karume (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Uhusiano wa Shirika la Ndege la Air Oman Philippe Georgious, wakati walipokutana katika chumba cha VIP kilichopo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jk Nyerere Dar es Salaam,Rais wa Zanzibara Abeid Karume alikuwa ametoka safari na PHilippe alikuwa amekuja hapo katika uwanja wa Ndege kuzindua upya usafiri wa ndege ya Air Oman kutoka Dar es Salaam na Oman wapilia (kulia)Mr Salm Al Hakamani ambaye ni mfanyabiashara wa oman na( watatu) Said Hamdoon Al Harthy mratibu wa usafirishaji.







No comments: