Welcome to pwaniraha blog please contribute by posting your comments on our blog, kindly note that abussive language is strictly not entertained. Thank you.
Welcome To Pwani Raha Blog; email us at "pwaniraha@gmail.com"

May 4, 2010

Wanao Ng'ang'ania Madaraka Katika Uongozi wa Soka Nchini.


Jamani watanzania na wapenda soka kwanini mnataka kutukosesha uhondo wa kuingia katika uwanja wa Taifa? kwanini watu mna ng'ang'ania kuwa viongozi? Rage umesha kuwa kiongozi wa iliyokuwa FAT akahujumu mali za shirikisho ukafungwa jela miaka 3 ukatoka kwa msamaham wa rais. Wambura umesha kuwa katibu mkuu wa iliyokuwa FAT lakini uchaguzi ulipofanyika wa TFF ulishindwa na uliondoka bila kukabidhi ofisi na nyaraka muhimu je kwanini bado huoni kama wanakandanda hawakuamini? kwani ni lazima uoiongoze Simba? Kaburou na wewe kwanini mnakuwa siyo waungwana? Kwanini msikubali mkawapa wagombea wote wakaingia katika uchaguzi ili atakayeshinda na kushidwa basi wote muwe mmeridhika. Hebu sasa angalieni Wambura anakwenda mahakamani ni dhahiri kuwa nchi yetu itafungiwa michezo ya kimataifa na tayari shirikisho lipo kwenye mchakato wa kumsaka mbadala wa Maximo. Inaonekana kwenye uongozi wa mpira Tanzania kuna masilahi mazuri au labda ndio mambo ya kujenga CV.

No comments: