Chama Cha Wananchi (CUF) kimelalamikia kitendo cha Diwani wa Kata ya Magomeni, Julian Bujugo (CCM) kwa kitendo cha kuitisha mikutano ya adhara na kisha kuwaada wananchi wa Kata hiyo ili apate kuchaguliwa tena nafasi ya Udiwani. Malalamiko hayo yalitolewa na baadhi ya wazee wa CUF katika kijiwe cha Shibam, wazee hao ambao hawakutaka kutaja majina yao gazetini walidai kuwa, kitendo cha Bujugo kuzunguka katika mitaa hiyo na wapambe wake ni kukiuka katiba ya Uchaguzi.
“Haiwezekani Bujugoo kuanza kuitisha mikutano ya adhara na kuongea mambo ya kujifagilia wakati hajasaidia chochote katika Kata hii” alisema Mzee huyo ambaye nji Kada wa CUF. Mwengine alisema kuwa, kitendo cha kujisifia kuwa ameweza kujenga barabara kwa kiwango cha lami huo ni uongo, wakati akijua ukweli barabara hiyo imejengwa chini ya kiwango kwa mradi wa Manispaa ya a Kinondoni na wala si yeye kama anavyojitangazia” alisema Mzee huyo. Mwandishi wa Habari hizi ambaye alikuwepo katika mkutanho huo uliofanyika mwishoni mwa wiki, ambapo Diwani huyo alikuwa akinadiwa na Makada mbalimbali wa CCM wa Kata hiyo akiwemo Mwenyekiti Shaweji Mkungura, walidai kuwa kwa kuona diwani wao huyo kuleta maendeleo Kata ya Magomeni wameamua kumchagua aendelee kugombea awamu nyingine. “Jamani Diwani wetu ametujengea barabara na ameweza kushirikiana na sisi kwa kila jambo hivyo tunaomba muendelee kumpa kura zenu za udiwani katika uchaguzi hapo baadae’ alisikika akimnadi Mwenyekiti huyo.
Hata hivyo baada ya kuwasiliana na Bujugo juu ya kushutimiwa kuanza kampeni mapema kabla ya wakati, hakuweza kupatikana baada ya simu yake kutokuwa hewani muda mrefu. Pia wazee hao walidai kuwa, kujitapa kuwa ameweza kutatua kero mbalimbali za Kata hiyo si kweli huku wazee hao wakisema kuwa, ameshindwa kuzuhia swala wanawake wanaojihusisha na biasahara ya Ukahaba tena nje ya shule yake kitendo ambacho wazee hao wamesema hawata kifumbia macho hata kidogo. “Kero kuu nyingi lakini kwa swala ili la kuwaacha hawa kufanyabiashara ya ukahaba ni fedhea kubwa, pia ameshindwa kuunda vikosi kazii ikiwemo ulinzai shilikishi, Sungusungu, kila siku Magomeni wananchi wanalalamikia kukabwa yeye ametekeleza yapi hapa” alihoji Kada huyo wa CUF.
2 comments:
I must digg your article so more folks are able to look at it, very useful, I had a tough time finding the results searching on the web, thanks.
- Mark
Very enlightening and beneficial to someone whose been out of the circuit for a long time.
- Lora
Post a Comment