Welcome to pwaniraha blog please contribute by posting your comments on our blog, kindly note that abussive language is strictly not entertained. Thank you.
Welcome To Pwani Raha Blog; email us at "pwaniraha@gmail.com"

May 20, 2010

Aliyenusurika Katika Ajali ya MV Bukoba Atunga Kitabu Kuhusu Tikio Hilo.


Mmoja wa wahanga waliokoka katika ajali ya Mv Bukoba iliyotokea Mei 21 siku ya Jumanne mwaka 1996 Nyaisa Simango ambaye kwa sasa ni Afisa Ugavi wa Benki Kuu ya Tanzania akionyesha kitabu alichotunga baada ya kunusurika katika ajali hiyo iliyouwa watu 800. Nyaisa kipindi hicho alikuwa mwajiriwa wa jeshi la Magereza kituo cha Ukonga jijini Dar es Salaam, wakati tukio linatokea alikuwa amempeleka mfungwa mkoani Kagera, kitabu hicho alichozindua kina kurasa 167, kikiwa na kichwa cha habari kisemacho SITASAHAU MV BUKOBA. Kulia ni Afisa habari mwandamizi wa Habari Maelezo Mwirabi Sise pia ni Mjomba wa Nyaisa kitabu kinapatikana katika bookshop mbali mbali hapa nchini kwa shilingi 12,000.



Baadhi ya wandishi wa habari wakiwa katika mkutano wa uzinduzi huo.



Nyaisa Simango akielezea jinsi alivyookoka katika ajari ya Meli ya Mv Bukoba.


Mmoja wa wanawake wanaofanya biashara ya mihogo na matango akimuuzia mmoja wa walemavu katika eneo la makutano ya barabara ya Ali Hassani Mwinyi na Uhio jijini Dar es Salaam, bidhaa hiyo imekuwa ikishamili kila kukicha kiasi cha kuwafanya wananchi wengi kushindia hiyo tu.

No comments: