Waziri Sofia Simba katikati akicheza ngoma ya asili.
.
Imeelezwa kuwa, Mwanamke mmoja hufa kwa ugonjwa wa Saratani kila baada ya sekunde moja Duniani kote.hususani walio na tatizo la Saratani ya Matiti. Hayo yalisema jana na Waziri wa Maliasili na Utalii,Shamsa Mwangunga katika matembezi ya Hisani ya kuchangia mfuko wa Saratani ya Matiti Tanzania ,iliyofanyika katika viwanja vya taasisi ya hospitali ya magonjwa ya kansa Ocean Road .
.
Katika hotuba yake hiyo, Shamsa ambaye alimwakilisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ambapo Mabalozi mbalimbali waliwakilisha katika matembezi hayo yaliyowakilisha pamoja na vikundi mbalimbali vya kijamii na wanafunzi waliotembea kwa mwendo wa kilometa 6 yakiongozwa na Mwangunga.
Katika Hotuba yake hiyo, Mwangunga aliitaka jamii kufunguka macho na kujitokeza kwa wingi kuangali afya zao na kutambua dalili za ugojwa huo mapema.
Katika matembezi hayo, Waziri Mkuu aliweza kuchangia shilingi Milioni tano huku kwa upande wake, Mwangunga alichangia mfuko huo kupipitia taasisi na idara ya wizara yake shilingi milioni nne.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chipukizi Wilya ya Kinondoni na Mwanaharakati wa kutetea haki za watoto nchini, Nimka Lameck (10) ambaye alikuwa maalum kutoa ujumbe kwa wananchi kuwa ugonjwa ni hatari hivyo kila mtoto anahaki ya kutoa ujumbe kwa jamii.
Naye Mkurugenzi na Mwanzilishi iwa Mfuko Asasi hiyo, Angela Kuzilwa aliwashukuru wadau mbalimbali walifanikisha katika taasisi hiyo pamoja na kutumikia Akina mam karibuni nchi nzima huku akitoa wito kwa wadau kujitokeza kuisaidia taasisi hiyo kwa michango ya hali na mali .
.
Taasisi hiyo ambayo makao yake makuu yapo jijini Dar es Salaam , Mwananyamala, inaendesha shughuli za ushahuri kwa waakina mama ilikujitambua na kushahuriwa kupima mapema ilikuepuka kupata matatizo makubwa huku matembezi hayo kwa mwaka huu yakifanyika kwa mara ya pili baada ya yale ya mwaka juzi.
Kwa upande wake Dkt Twalib Ngoma wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road , aalitoa wito kwa akina mama kujitokeza kwa wingi kuchunguzwa afya zao ilikujijua mapema kama wameambuzaikwa au la, “ Tunawaomba akimama kujitokeza kwa wingi kupima afya juu ya ugonjwa huu mapema ilikuondoa ukubwa wa tatizo” alisema Dkt Ngoma. Huku mlezi wa taasisi hiyo, mke wa rais wa awamu ya tatu, Anna Mkapa alitoa wito kwa taasisi mbalimbali kujitokeza na kuichangia ilikupunguza kwa asilimia kubwa ya ugonjwa huo ambao unawapata akina mama walio na umri wa miaka 40 na kuendelea pamnoja na idadi ndogo ya wanaume
1 comment:
nike air max
balenciaga shoes
golden goose sneakers
moncler
yeezy boost 500
calvin klein outlet
vans shoes
supreme clothing
christian louboutin outlet
yeezy shoes
Post a Comment