Welcome to pwaniraha blog please contribute by posting your comments on our blog, kindly note that abussive language is strictly not entertained. Thank you.
Welcome To Pwani Raha Blog; email us at "pwaniraha@gmail.com"

February 27, 2010

Simba Dimbani Leo Na Zesco.

Timu ya soka ya Simba leo itajitupa uwanjani kumenyana na Zesco ya Zambia katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Awali, Zesco, washindi wa pili wa Zambia, nyuma ya mabingwa Zanaco, walikuja Tanzania kwa lengo la kuinoa Yanga ambayo leo ipo Lubumbashi kumenyana na FC Lupopo katika mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Kwa mujibu wa msemaji wa Simba, Cliford Ndimbo, mechi hiyo itatumiwa na timu yake kama ni sehemu ya maandalizi ya mechi yao ya kombe la Shirikisho wakati wakisubiri mshindi kati ya na As Adema ya Madagascar na Lengthenes ya Zimbabwe baadaye mwezi ujao.
.
Lakini pia, kocha Patrick Phiri ataitumia mechi hiyo kurejesha imani ya wapenzi na wadau wa Simba, ambao waliishuhudia timu yao ikipepesuka na kuambulia sare ya bao 1-1 huku ikionyesha kiwango kibovu kiasi cha kulalamikiwa katika mechi yao dhidi ya Yanga iliyochezwa Jumanne. Zesco walitoka sare ya bao 1-1. Bao la Wazambia hao liliwekwa kimiani na Billy Mwanza wakati lile la kusawazisha lilifungwa na Kiggy Makasy.Kocha wa Zesco, Fighton Simukonda alisema kuwa ameahidi kucheza kikosi imara ambacho kitaondoka na ushindi katika mechi hiyo ambayo nao wanaitumia kwa maandalizi ya mechi za kimataifa.
.
Kikosi cha Simba ambacho muda huu kitajitupa uwanjanai kucheza mechi ya kirafki na timu ya Zesco ya Zambia katika uwanja wa Uhuru.

Sista wa kituo cha Afya cha Buguruni akimpima uzito mtoto Hamis Juma mwenye umri wa miezi 7 ambaye alikuwa na uzito wa kilo 9 kulia ni mama yake mzazi Mwajuma Juma akishuhudi.

No comments: