Welcome to pwaniraha blog please contribute by posting your comments on our blog, kindly note that abussive language is strictly not entertained. Thank you.
Welcome To Pwani Raha Blog; email us at "pwaniraha@gmail.com"

June 17, 2010

Wanawake Watoana Jasho Katika Kijiji Cha Kisasa.


Miss Tedy akifurahia baada ya kafanikiwa kutumbukiza kete tatu kwa wakati mmoja haya yote ndani ya kijiji cha pool tandika Davis corner.

Miss Manka Mushi akijitahidi kusawazisha baada ya kufungwa 3 kwa 1 na Miss Jack hayupo pichani.

Miss edina Kimaro akishangaa kumuona mpinzania wake akimalizia kete na yeye  za kwake zipo kibao .
.
Haya yote na mengine kibao yanapatikana ndani ya kijiji cha pool  akizungumza baada ya mechi hizo mkurugenzi wa kijiji hicho, bwana Emmanuel  Mwakabana  amesema mashindano hayo huwa yanafanyika mara kwa mara  na kwa timu zinazoshiriki ni mbalimbali na zinatoka wilaya zote na vitongoji vyake . Mwakabana amesema anapenda kuchukua afasi hii kuwaomba wapenzi na wachezaji ndani na nje ya temeke kuja  ndani ya kijiji na kuukuza mchezo huu zaidi alisema mwakabana.
.
Alisisitiza zaidi kupata wadhamini zaidi  na kuyaomba makampuni na mashirika mbalimbali yajitokeze na kudhamini mchezo huu “mchezo wa pool ni sawa na michezo mingine ambayo inapata sapoti kutoka serikalini na hata kwa mheshimiwa Rais sasa nachukua nafasi hii kuiomba wizara ya michezo kuangari kwa jicho la tatu mche huu “.