Pages

November 9, 2009

Ndege ya Miraa (Mrungi/Veve) Yaanguka Nairobi na Kuua Wawili.

Ndege moja nchini Kenya iliyokuwa imebeba miraa kupeleka Somalia, imeanguka baada ya kupata hitilafu la kiufundi ambapo ilimlazimu rubani aitue ndege hiyo muda mfupi tu baada ya kupaa. Katika jaribio la kutua ndege ndipo ndege hiyo iligonga uzio wa kiwanja cha ndege na kulipuka. Rubani wa ndege hiyo alifariki alipokuwa anapelekwa hospitalini na msaidizi wake alifia hospitali akipata matibabu.

No comments:

Post a Comment