
Kutoka kulia ni Meneja Masoko wa Vodacom Tanzznia Upendo Richard akiwakabidhi ufunguo wa pikipiki washindi wa shindano la Samsung Nimesh Solawa katikati na Yasin Karim wa Kampuni ya Ram Group of Campaness Limited baada ya kuwa wateja wakubwa wa kununua simu nyingi za Samsung. Hafla hiyo ilifanyika katika ofisi za Vodacom zilizopo katika jengo la PPF Tower Dar es Salaam.

kutoka kulia Meneja Masoko wa Vodacom Upendo Richard akimuonyesha simu iliyokuwa na ujumbe wa kuionyesha kiasi cha pesa alizoshinda Joyce Andrew kushoto akiwa na mtoto wake mwenye umri wa miezi 4 Traves Hope ,kiasi cha shilingi milioni 1.6.

Mmoja wa wahindi katika shindano la kununua simu za samsung linaloendeshwa na Vodacom akikabidhiwa simu yenye ujumbe wenye zawadi ya shilingi milioni 1.6 na Meneja Masoko wa Vodacom Upendo Richard.

Kushoto Jasinya Boniface ambaye ni Trade Marketing officer wa Vodacom na Upendo Richard Trade Marketing Manager wa Vodacom wakitoa maelezo wakati walipokuwa wakiwakabidhi washindi wa shindano la kununua vifaa na Simu za Samsung ambapo jumla ya washindi wanne wakazi wa jijin la Dar es Salaam kila mmoja alijishindia mkiasi cha shilingi Milioni 1.6. Shindano kubwa la mchezo huo litafanyika tarehe 13 mwezi huu na mshindi atajinyakulia kiasi cha shilingi milioni 13.
No comments:
Post a Comment