Welcome to pwaniraha blog please contribute by posting your comments on our blog, kindly note that abussive language is strictly not entertained. Thank you.
Welcome To Pwani Raha Blog; email us at "pwaniraha@gmail.com"

September 19, 2009

Obama Calls Kanye West A Jack Ass





Hivi majuzi mwanamuziki wa miondoko ya hip hop Kanye West alimpokonya kipaza sauti (mic) mwanadada mmoja ambaye alikuwa ameshinda best video kwenye MTV awards. Kanye aliibuka kwenye jukwaa akidai kuwa Beyonce ndio anastahili ushindi huwo. Baadaye Kanye alimrudishia "mic" huyo dada lakini mwanamuziki huyo alishindwa kuongea kutokana na kitendo alichofanyiwa na Kanye.

Kanye alimtoa nishai hadharani huku umati wa watu ukiangalia kwenye TV. Mwanamuziki huyo alikuwa anatoa shukrani zake wakati aliposhinda tuzo hiyo na ghafla tu Kanye akampokonya mic na kumsifia Beyonce. Alipomrudishia "mic" mwanadada huyo alishindwa kusema chochote. Watu wengi walichukizwa na kitendo cha Kanye, miongoni mwao akiwa Barack Obama.

Obama alikuwa anajiandaa na interview ya televisheni kupitia kituo cha CNN ndipo alipoponyokwa na mdomo na kumwita Kanye West kuwa ni "Mpumbavu flani" (Jack Ass). Obama alidhani kuwa kamera zilikuwa hazijaanza kurekodi.