Welcome to pwaniraha blog please contribute by posting your comments on our blog, kindly note that abussive language is strictly not entertained. Thank you.
Welcome To Pwani Raha Blog; email us at "pwaniraha@gmail.com"

September 21, 2009

Mambo ya Sherehe za Iddi katika Pwani ya Dar es salaam.

Wanenguaji wa bendi ya Extra Bongo (next level) wakifanya vitu vyao katika onyesho lililofanyika katika ukumbi wa Mango Garden Kinondoni.

Watalaam wa kung'uta gita wa bendi ya Extra Bongo kutoka kushoto ni Kamodee akipiga bass, Glegory Salekinda akipiga Solo, Adamu Hussein (Mkono wa rushwa)akilicharaza solo na Israel Bush akilicharaza rthym wakati wa onyesho lao la kwanza tangua walipoitambulisha bendi hiyo mwezi Augosti katika ukumbi wa Msasan i Club. Katika onyesho la jana ukumbi ulifurika kiasi cha kutapika na kukukosa sehemu ya kukanyanga hivyo wapenzi wa muziki kwa niaba ya msemaji wa Extra Bongo Deugratus Sagawala anawashukuru sana mashabiki waliofika kuipa sapoti bendi ya wazawa.

Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakisherehekea sikukuu ya Idd el Fitri katika ufukwe wa Coco Beach sehemu hii imekuwa kivutio kwa wakazi wa maeneo ya jiji kutokana na ufukwe huo kuwa bado unamilikiwa na serikali, sehemu kama hizi nyingi zimeuzwa na hivyo kuwafanya watanzania kukosa sehemu ya kupumzikia. wote tunawatakia Idd njema.

Wanenguaji wa bendi ya African Stars Twanga Pepeta wakonyesha umahiri wao katika onyesho lililofanyioka katika ukumbi wa LandMark Hotel ikiwa ni sehemu ya shamra shamra ya sikukuu ya Idd.

Jamani mmeniona? mwanamuziki Banza Stoni akijiandaa kumkabidhi zawadi mmoja wa watoto walioshinda zawadi ya kucheza vizuri wakati wa shindano la watoto lililofanyika katika ukumbi wa Mango Garden lililokuwa limeandaliwa na bendi ya ExtraBongo ikiwa ni sehemu mojawapo ya kusherehekea sikukuu ya Idd el Fitr. Banza kwa siku za nyuma alikuwa mgonjwa sana kiasi cha taarifa kuzagaa kuwa amefariki lakini tunamshukuru Mungu kwa kuendelea kumlinda na sasa hali yake inaendelea vizuri wapenzi na mashabiki wake jana walifurahia sana baada ya kumuona akiwa jukwaani akitoa zawadi na kuonyesha ushirikiano mzuri kwa rafiki yake Ali Choki.

1 comment:

Nautiakasi said...

Hakukosea mwenyewe alipoimba "hujafa hujasifiwa.." Wanamsubiri afe ndo waamsifu kiunafiki, wamemzulia kila baya hata kufika hatua ya kumtangazia amefariki..lakini Mungu amemsimamisha tena..ooh nachechemea