Welcome to pwaniraha blog please contribute by posting your comments on our blog, kindly note that abussive language is strictly not entertained. Thank you.
Welcome To Pwani Raha Blog; email us at "pwaniraha@gmail.com"

September 15, 2009

Mpakanjia Afariki Dunia

Mfanyabiashara maarufu na mdau mkubwa wa michezo na burudani nchini, Mohamed Mpakanjia amefariki dunia jana katika hospitali ya jeshi la Lugalo jijini Dar es Salaam.Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana katika hospitalini hiyo ambayo pia alifikia aliyekuwa mkewe Amina Chifupa, Mpakanjia amefariki dunia katika hospitali hiyo majira ya saa saba mchana.Chanzo chetu cha habari kilichopo katika hospitali hiyo kilisema kuwa mfanyabiashara huyo alifikishwa hopitalini hapo jumamosi iliyopita kutokana na kusumbuliwa na homa ya mapafu."Aliletwa hospitalini hapa jumamosi akisumbuliwa na matatizo ya homa ya mapafu. Wakati analetwa alionekana mwenye afya njema lakini hali yake ilibadilika ghafla leo na mauti kumfika," kilisema chanzo hicho cha habari.Katika uhai wake Mpakanjia alikuwa ni miongoni mwa watu waliotoa mchango mkubwa katika maendeleo ya michezo na burudani hasa kutokana na kusaidia wasanii, wanamuziki na bendi nyingi za muziki hapa nchini.Alikuwa mfadhili mkuu wa bendi ya DDC Mlimani Park 'Sikinde', Tanzania One Theater 'TOT Plus' na bia alidhamini albamu za pamoja za wanamuziki Ramadhani Masanja 'Banza Stone', Ally Choki na kiongozi wa Msondo iitwayo 'Sisi ndiyo Sisi' ya mwaka 2005.Kwa upande wa sanaa alitoa mchango mkubwa kwa kuwasaidia wasanii wengi wa sanaa ya filamu na maigizo kwa kuwawezesha kifedha kukamilisha kazi zao hizo. Mungu ailaze roho yake pema peponi. Amina

2 comments:

Anonymous said...

R.I.P

Simon Kitururu said...

R.I.P!