Welcome to pwaniraha blog please contribute by posting your comments on our blog, kindly note that abussive language is strictly not entertained. Thank you.
Welcome To Pwani Raha Blog; email us at "pwaniraha@gmail.com"

August 3, 2009

Kumbe Obama Amezaliwa Mombasa Kenya

Hichi cheti cha kuzaliwa kinasadikiwa kuwa cha rais Obama.

Cheti kinavyoonekana kwa karibu.

Hapa ni kwa chini.

Katika jamii ya mtandao (internet) kuna fununu kuwa Rais wa Marekani Barack Hussein Obama alizaliwa katika hospitali ya Coast General Mombasa. Kuna watu wamepiga picha cheti hicho, ilikuionesha jamii katika ulimwengu wa mtandao kuwa urais wa Obama ni batili kwasababu ni Mkenya. Cheti hicho kinaonesha kuwa Obama amezaliwa tarehe 4 Agosti 1961, vilevile kinaonesha kimetengenezwa tarehe 17 Agosti 1964.
.
Unkikiangalia cheti hicho kwa juu juu unaweza kudhani shtuma hizi ni za kweli, lakini kuna mambo mengi hayajakaa sawa. Mwaka 1961 kulikuwa hakuna jamuhuri ya Kenya, bado mkoloni alikuwa anatawala Kenya. Coast Province (Mkoa wa Pwani) ilianzishwa 1970, kabla ya hapo Kenya ilikuwa imegawanywa katika Region na sio Province. Hii inaonyesha wazi kuwa cheti kilechoandaliwa 1964 na Coast Province ya Kenya ni uwongo mtupu. Cheti chenyewe kipo safi utadhani kimetolewa miaka ya tisini. Pia kwa uzoefu wangu, vyeti vya kuzaliwa hutolewa kwa mfumo wa "Landscape" na sio "Portrait" kama cheti hichi.

1 comment:

Anonymous said...

Can you ask someone who was born at Mombasa in 1961, if this Certificate of Registration looks authentic?

Sara Obama has said that Barack Hussein Obama II was born at Mombasa...