Welcome to pwaniraha blog please contribute by posting your comments on our blog, kindly note that abussive language is strictly not entertained. Thank you.
Welcome To Pwani Raha Blog; email us at "pwaniraha@gmail.com"

July 15, 2009

Timu ya Mjini Magharibi

Mshambuliaji wa timu ya Mkoa wa Mjini magharibi Juma Mbwana akiruka daruga la beki wa Kigoma, Swaleh Hamis Nasibu katika mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Copa Coca Cola uliofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, jana. Mjini Maghari ilishinda 2-0.
Timu ya Mjini Magharibi leo imetinga nusu fainali ya mashindano ya Copa Coca Cola baada ya kuinyuka timu ya Kigoma kwa mabao mawili kwa bila. Timu hiyo imekuwa kivutio kikubwa sana kwa kutandaza kandanda ya uhakika katika mashindano hayo.
Baada ya mchezo huo timu hiyo ilishangilia kwa kuwabeza wakazi wa Dar es salaam kwa kuwaimbia wimbo ulisikika kuwa "mnatusema sisi mdebwedo sasa mtatukoma" hii inatokana na kundi la kuchekesha Orijino lililoanzisha mchezo wa mdebwedo kwa watu wa Zanzanibar. Kesho kutakuwa na nusu fainali nyingine kati ya timu ya morogoro na timu ya tabora mpambano huo unategemea kuwa wa vuta ni kuvute hasa kutokana na timu hizo kuonyesha viwango vya hali ya juu katika michuano hiyo.

No comments: