July 25, 2009
Nyoshi awagombeza Wanenguaji Wake.
Rais wa bendi ya FM Academia Nyoshi Alsadat jana aliwafokea wanenguaji wake wakati wa walipo shuka kutoka kwenye jukwa katika onyesho la uzinduzi wa bendimpya ya Five Star Modern Taarab ambao ulifanyika katika ukumbi (uwanja) wa New Msasani Club.
Nyoshi aliwafuata wanenguaji nyuma ya jukwaa na kuanza kuwaporomoshea matusi kwa kitendo chao cha kucheza chini ya kiwango jambo ambalo lilionekana kumkera sana kiongozi huyo.
Hata hivyo wanenguaji hao walionekana kuchukizwa na kitendo hicho cha kuwafokea hadharani badala ya kuwaeleza kiustarabu. "Hii sio tabia nzuri yeye anasea hatujachangamuka jukwaani alitakatufanyeje?" alisema mmoja wa wanenguaji ambae jina lake linahifadhiwa. Stori zaidi....
Nyoshi ambaye kila siku anaonekana akiwa amevalia suti mpya huku zikiwa na lebo ya dukani pasipo kuchanwa inamaanisha kuwa huwa anaazima au vipi maana nguo ukiinunua dukani lazima uchane lebo la sivyo utaonekana mshamba. Hata hivyo FM iliwapagawisha mashabikmi waliofurikakatika ukumbi huo kama kawaida ya wazee wa mapamba hawakufanya kosa walitoa burudani tosha.
Sabrina, Mariamu na Sharon wakionyesha umahiri ambao haukumkuna bosi wao.
Sharon anajipinda vilivyo lakini bosi hajafurahi.
Mpiga tumba Seif Mbonde pembani ni dansa Titina Mwinyi wakishughulika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment