Welcome to pwaniraha blog please contribute by posting your comments on our blog, kindly note that abussive language is strictly not entertained. Thank you.
Welcome To Pwani Raha Blog; email us at "pwaniraha@gmail.com"

July 16, 2009

Mpangaji atupiwa Vitu Vyake Nje

Rose akikagua vyitu vyake vilivyotupwa nje na mwenye nyumba wake.

Kijana huyu anakagua kama CD zote vipo. Sipati picha kama ingekuwa Kinondoni ingekuwaje, hata sisi tusingeweza kupiga picha maana pasinge kuwa na vitu.

Hili ndilo Kanisa lililo pangishwa, wenyewe wanajiita the Mega Church.
Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Rose ambaye alikuwa amepanga katika nyumba namba 104 iliyoko katika mtaa wa Nyuma Mikocheni B, amejikuta katika wakati mgumu baada ya mwenye nyumba wake kumtolea vitu vyake vya thamani nje bila ya taarifa wala ridhaa yake.

Rose alimuaga mama mwenye nyumba wake (Joyce Mbuga) kuwa anaenda Mbeya kumuangalia mwanawe aitwaye Jennifer (14) mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya secondary ya Elimuladi ambaye alikuwa amevunjika mguu na alihitajika ahamishwe kutoka hospitali ya Wemba Mission kuja Muhumbili kwa matibabu zaidi. Wakati akiwa Mbeya mama mwenye nyumba alikuwa akimpigia simu Rose aje atoe vitu vyake katika chumba chake.

Rose akiongea na mwandishi wa habari hizi alisema tayari walikuwa na makubaliano ya kupanga katika nyumba hiyo ambapo kwa muda wa miezi minne tayari alikuwa amesha mlipa mama mwenye nyumba hiyo kiasi cha Tsh. 400,000. jambao ambalo walikuwa wamekubaliana awali lakini mama mwenye nyumba huyo alipata wateja wengine waliopenda kupanga katika eneo hilo kwa nia ya kufanya kanisa. Mpaka sasa chumba hicho tayari kimepangishwa watu ambao sio raia wa Tanzania na wameanzisha kanisa linalojulikana kwa jina la Kanisa la Kimataifa la Light House Chapel likiwa na ujumbe usema The Mega Church (Kanisa Kubwa). Baada ya mama huyo kupangisha nyumba hiyo kwa watu wa kanisa, alimtolea mpangaji wake Rose vitu vyake vyote nje na kufanya viibiwe pasipo yeye kujua wakati akiwa hospitalini Muhimbili.

Kutokana na tatizo hilo mjumbe wa nyumba kumi katika eneo hilo alipata taarifa na kusema kuwa kitendo alichofanya mama Joyce si chakiungwana. Hadi sasa dada Joyce ameswekwa ndani katika kituo cha polisi Oyster Bay jijinii.

1 comment:

Anonymous said...

Thanks for an idea, you sparked at thought from a angle I hadn’t given thoguht to yet. Now lets see if I can do something with it.