Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom leo imemkabidhi mshindi wa shindano hilo la Tuzo Milionea Bwana Renatus Mkinga kiasi cha shilingi milioni 100 Mkurugenzi wa masoko wa vodacom Ephraim Mafuru wakati akimkabizi mshindi huyo alisema kuwa Mkinga alishinda pesa hizo kupitia Promosheni ya Tuzo Milionea iliyodumu kwa miezi kumi na moja. Promosheni hiyo ni mwendelezo wa programu ya tuzo pointi Droo, ambayo alisema ililenga kawapa wateja wa Vodacom Tanzania zawadi mbalimbali kama vile muda wa maongezi simu na fedha taslimu.
Kampuni ya Vodacom ilianzishwa miaka tisa iliyopita na shindano la Tuzo ni shukrani kwa watanzania kwa kusema asante wakati huo huo mshindi wa shindano hilo Renatus ambaye jana alikabidhiwa kitita hicha cha milion 100 alisema kuwa yeye siku ya mchezo alikuwa anaelekea kwenda kunywa pombe pamoja na wafanyakazi wenzake lakini wakati wakiwa njiani alibadili mawazo na kuamua kwenda nyumbani .
Wakati akiwa nyumbani muda wa saa 2. alimwomba mkewe amchajia simu yake ambayo ilikuwa imikwisha chaji. baada ya hapo alikwenda kuangalia TV kipindi cha kuchezesha mchezo huo jambo ambalo kwake halikuwa kitu cha kawaida ndipo alipopigiwa simu kuwa ameshinda.
No comments:
Post a Comment